ZAMBIA-SIASA-UCHAGUZI

Rais wa Zambia awasihi majaji kutoiga majaji wa Kenya

Rais wa Zambia, Edgar Lungu.
Rais wa Zambia, Edgar Lungu. DR

Rais wa Zambia Edgar Lungu amewaonya majaji nchini humo kutoiga majaji wa Kenya kutokana na hofu ya kuzuka vurugu iwapo watachukua uamuzi wa kumzuia kushiriki uchaguzi wa urais wa mwaka 2021.

Matangazo ya kibiashara

Kauli hii inakuja baada ya kuzuka mjadala kuhusu kuwania au la kwa Edgar Lungu katika uchaguzi wa mwaka 2021.

Wakosoaji wake wanasema kwamba Bw Lungu anahudumu muhula wa pili. Kulingana na Katiba ya Zambia rais anaruhusiwa kuhudumu kwa mihula miwili pekee kwa mujibu wa katiba nchini humo..

Wanasema kipindi ambacho alihudumu baada ya kifo cha Rais Michael Sata mwaka 2014 kinafaa kuhesabiwa kama muhula wa kwanza.

Hali hii inafanana na ile ya Burundi, ambapo rais Pierre Nkurunziza alikataa kuwa mwaka 2005 hakuchguliwa na raia na ndio maana muhula wake wa miaka mitano tangu 2005 hauwezi kuhesabiwa kama muhula.

Kambi inayomuunga mkono Bw Lungu wanabaini kwamba alimaliza tu muhula wa mtangulizi wake na kwamba muhula wake wa kwanza ulianza baada ya ushindi wake wa uchaguzi wa ,waka 2016.