SENEGAL-CLAUDE-GHISLAINE-VYOMBO VYA HABARI

Tuzo ya Dupont-Verlon yatunikiwa raia 2 wa Senegal

Cécile Mégie, mkurugenzi wa RFI (kushoto), Apolline Verlon, binti ya Claude Verlon, pamoja na washindi wa tuzo ya Dupont-Verlon A.Diouf na N.Diedhiou, Bi Poinsot, mama wa Ghislaine Dupont, balozi wa Ufaransa Christophe Bigot, Marie-Christine Saragosse , Mk
Cécile Mégie, mkurugenzi wa RFI (kushoto), Apolline Verlon, binti ya Claude Verlon, pamoja na washindi wa tuzo ya Dupont-Verlon A.Diouf na N.Diedhiou, Bi Poinsot, mama wa Ghislaine Dupont, balozi wa Ufaransa Christophe Bigot, Marie-Christine Saragosse , Mk Abdoulaye Diaw

Siku ya Alhamisi ilikuwa kumbukumbu ya miaka 4 ya mauaji ya waandishi wa habari wa RFI Claude Verlon na Ghislaine Dupont ambao walitekwa na baadae kuuawa katika mji wa Kidal kaskazini mwa Mali. Ili kuwaenzi waandishi hao, RFI hutoa tuzo iliobeba majina ya waandishi hao ijulikanayo kama "Bourse Dupont Verlon".

Matangazo ya kibiashara

Baada ya Mali, Madagascar na Benin mwaka huu wa 2017 ilikuwa ni zamu ya Senegal ambapo kwa mara ya kwanza bourse ya fundi mitambo imepewa mwanamke Nicole Diedhiou ambae alidhihirisha furaha yake baada ya kutangazwa mshindi.

“Nataka kuwashukuru wote, hususan mtu mmoja alienishawishi kushiriki, yupo hapa Marie Joseeph, nataka kusema kwamba tulikuwa 10 ni kweli kwamba nilikuwa mwanamke pekee, lakini wote kumi sio kwamba hawakustahili, ninaamini kwamba wote ni washindi pia”, alisema Nicole Diehiou.

Tuzo ya mwandishi wa habari ilipewa Arona Diouf baada ya ripoti yake kuhusu maradhi ya fistula yanayowakumba wanawake jijini Dakar na ambae naye kwa furaha amepongeza waandaji wa tuzo hiyo.

“Nawashkuru wote, kampuni ya France Media Monde, heshima pia zinawaendee watu wa familia ya Ghislaine Dupon na Claude Verlon, mnazungumzia ugonjwa huo unawakabili kina mama nchini Senegal, ilikuwa ni kutaka kuonyesha dhiki ya kina mama nchini Senegal wanaokumbwa na maradhi hayo”, amesema Arona Diouf.

Tangu kutokea kwa kifo cha Ghislaine Dupon na Claude Verlon Novemba 2, tarehe hii iliidhinishwa na Umoja wa Mataifa kuwa siku ya kimataifa ya kupinga unyanyasaji dhidi ya waandishi wa habari na hali ya kutowaadhibu wahusika wa unyanyasaji huo.

Wakili wa mama wa Ghislane Dupon Valerie Courtois anasema kesi hiyo imepiga hatuwa, ingawaje sio kuwa sana.

“Katika miezi ya hivi karibuni kumepigwa hatuwa, maana jaji aliomba baadhi ya taarifa moja kwa moja kutoka Umoja wa Mataifa, minusma, ilikuw ani muhimu kupata taarifa hizo kuhusu hali ilivyokuwa kabla na baada ya kutekekwa na kuawa kwa ghislaine Dupon na Claude Verlon”, amesema mamake Ghislaine Dupont.

Ni siku ambayo imekuja wakati katika mataifa mbalimbali waandishi wa habari wameendelea kunyimwa haki ya kutekeleza kazi yao kama kawaida.