DRC

CENI kutangaza kalenda ya uchaguzi mwishoni mwa juma hili

Balozi wa Marekani kwenye umoja wa Mataifa Nikki Haley akiwa na rais wa  tume ya uchaguzi DRC CENI, Corneille Nangaa,jijini Kinshasa  27 Oktoba 2017.
Balozi wa Marekani kwenye umoja wa Mataifa Nikki Haley akiwa na rais wa tume ya uchaguzi DRC CENI, Corneille Nangaa,jijini Kinshasa 27 Oktoba 2017. REUTERS/Robert Carrubba

Tume Huru ya Uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo-DRC, CENI inatarajiwa kutoa kalenda ya uchaguzi mwishoni mwa juma hili licha ya Tume hiyo hapo awali kutoa angalizo kuwa uchaguzi hauwezi kufanyika kabla ya mwaka 2019.

Matangazo ya kibiashara

Hayo yanajiri wakati huu hali ya joto la kisiasa ikiendelea kupanda kwa Rais Joseph Kabila kutakiwa kuondoka madarakani kwa kuheshimu makubaliano ya Desemba 31 mwaka jana huku Marekani ikishinikiza uchaguzi ufanyike 2018.

Hivi karibuni Naibu Mwenyekiti wa CENI, Norbert Basengezi ameripotiwa akisema kuwa ukalenda ya Uchaguzi itatolewa mwishoni mwa juma hili na kwamba makubaliano ya Desemba 31 yataheshimiwa.

Norbert Basengezi amesema kuwa tayari tume yake imekutana na wajumbe wa kamati inayoratibu utekelezwaji wa makubaliano hayo pamoja na wajumbe wa serikali ili kuafikiana kuhusu kalenda ya uchaguzi.