LIBERIA-UCHAGUZI-SIASA

Mahakama Kuu yasimamisha mchakato wa uchaguzi Liberia

Majaji wa Mahakama Kuu ya Liberia. Katikati,rais anayemaliza muda wake, Ellen Johnson Sirleaf.
Majaji wa Mahakama Kuu ya Liberia. Katikati,rais anayemaliza muda wake, Ellen Johnson Sirleaf. Supreme Court of Liberia

Mahakama ya Juu nchini Liberia imesimamisha mchakato wa uchaguzi nchini humo siku moja kabla ya kufanyika kwa duru ya pili. Duru ya pili ya uchaguzi wa urais ambao ungeuliwakutanisha nyota wa zamani wa soka George Weah akipeperusha bendera ya muungano wa CDC (Coalition for Democratic Change), na Makamu wa rais Joseph Boakai.

Matangazo ya kibiashara

George Weah alishinda kwa 38.4% ya kura katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais uliofanyika Oktoba 10, Makamu wa rais anayemaliza muda wake Joseph Boakai alichukua nafasi ya pili akipata 28.8% ya kura.

Hivi karibuni chama cha upinzani cha Liberty kilichochukua nafasi ya tatu kwa 9.6% ya kura kiwasilisha malalamiko yake mahakamani kikidai kuwa duru ya kwanza ya uchaguzi iligubikwa na udanganyifu wa kura, kikinyooshea kidole cha lawama tume ya uchaguzi nchini Liberia kupotosha matokeo ya uchaguzi.

Chama tawala nchini Liberia kimewasilisha malalamiko rasmi dhidi ya tume ya uchaguzi kuhusu matokeo ya uchaguzi wa rais wa Oktoba 10, siku kadhaa kabla ya duru ya pili inayomhusisha mgombea wake, Makamu wa Rais Joseph Boakai na mpinzani George Weah aliyeibuka mshindi.

Chama tawala cha Unity Party kilitishia kuungana na vyama vingine viwili kutafuta "muafaka wa kisheria haraka iwezekanavyo chini ya sheria za Liberia, kufuatia chama cha Liberty na chama cha All Liberian Party (ALP) kufungua malalamiko na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Kiongozi wa chama cha upinzani cha Liberty, Charles Brumskine, alikwenda mahakamani kutaka Makamishena wa Tume ya Uchaguzi kuondolewa kazini.

Hivi karibuni Bw. Brumsike alisema Makamishena hao walihusika na wizi wa kura.

Aidha, alisisitiza kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jerome Korkoya, na wenzake wamekosa uaminifu wa kusimamia Uchaguzi utakaokuwa huru na haki.

Taarifa iliyotolewa na vyama vitatu ikiwa ni pamoja na chama tawala cha Unity Party inasema uchaguzi, ambao nyota wa zamani wa soka la kimataifa George Weah aliongoza kwa kura nyingi kati ya wagombea 20, ulitawaliwa na udanganyifu mkubwa wa kimfumo.