DRC-OIF-UCHAGUZI

OIF yaonya dhidi ya kutoheshimisha kalenda ya uchaguzi DRC

Pascal Couchepin, Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa La jumuiya ya nzhi zinazozungumza Kifarans (OIF) kwa Ukanda wa Maziwa Makuu.
Pascal Couchepin, Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa La jumuiya ya nzhi zinazozungumza Kifarans (OIF) kwa Ukanda wa Maziwa Makuu. (Photo : Fabrice Coffrini/AFP)

Pascal Couchepin, Mjumbe maalum wa Jumuiya ya nchi zinazozungumza Kifaransa (OIF) kwa Ukanda wa Maziwa Makuu ameonya serikali na tume ya uchaguzi nchini DRC dhidi ya kutoheshimu kalenda ya uchaguzi.

Matangazo ya kibiashara

Jumuiya ya nchi zinazozungumza Kifaransa (OIF) ina wasiwasi kuhusu wito wa kuandamana unaotolewa na upinzani pamoja na vyama vya kiraia, huku ikitolea wito serikali ya DRC kuwa makini na hali hiyo. Kama pamoja na Kalenda hiyo, raia wakiona kuwa walidanganywa, kutakua na hali ya kutisha, " alionya Bw Couchepin.

Kauli hiyo aliitoa siku ya Jumapili wakati akihitimisha ziara yake ya siku nne nchini DR Congo.

Bw Couchepin alikutana na wawakilishi wa vyama vinavyomuunga mkono rais Joseph Kabila, upinzani, Tume ya Uchaguzi (CENI) na Baraza kuu la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (Cenco), Spika wa Bunge, lakini hakuweza kukutana na Rais Joseph Kabila. Kwa mujibu wa rais wa zamani wa Shirikisho la Soka la Uswisi, kuchapishwa kwa kalenda ya uchaguzi wiki iliyopita ni "jambo zuri". Kinachobaki ni kupata uhakika kuwa itatekelzwa, vinginevyo,"kunaweza kukatokea mlipuko mkubwa na hali kuwa mbaya zaidi kuliko inavyoshuhudiwa wakati huu nchini humo," Mjumbe wa Jumuiya ya nchi zinazozungumza Kifaransa alionya.

Pascal Couchepin hakuweza kukukutana na Rais Kabila, ambaye yuko ziarani katika mikoa ya nchi hiyo.

Kundi la wataalam kusaidia Ceni

Hata hivyo OIF ina matumaini. Katika jaribio la kurejesha uaminifu, OIF inaomba kuwekwa kundi la wataalam wa kimataifa watakaosaidia Tume ya Uchaguzi (CENI) katika utekelezaji wa kalenda ya uchaguzi. Sheria ya kamati hii tayari ilipitishwa New York Septemba katika kando ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, lakini bado haijaanza kutekelezwa. EU, AU, OIF, ICGLR na SADC tayari wamekubali kushiriki kwenye timu hiyo, lakini sio wadau wote wanakubaliana kuhusu sheria na mamlaka yake.

Wakati huo huo mvutano unaendelea kati ya jumuiya ya kimataifa na Tume ya Uchaguzi kuhusu suala la ufadhili wa uchaguzi. "Wadhamini hawawezi kutoa fedha zao kabla ya kupata hakikisho kwamba uchaguzi utafanyika, alibaini Pascal Couchepin.