DRC-HAKI

Kesi ya ubakaji watoto kuendelea kusikilizwa Kavumu, DRC

Wanamgambo 18 ikiwa ni pamoja mbunge Frederic Batumike wanashtumiwa kuwabaka wasichana zaidi ya 46 katika kijiji cha Kavumu, mashariki mwa DRC.
Wanamgambo 18 ikiwa ni pamoja mbunge Frederic Batumike wanashtumiwa kuwabaka wasichana zaidi ya 46 katika kijiji cha Kavumu, mashariki mwa DRC. Google Maps

Wanamgambo 18 wanatazamiwa Jumanne hii Novemba 14 kufikishwa mbele ya mahakama iliyoko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa ajili ya kusikiliza mashtaka yanayowakabili ya kuwabaka zaidi ya watoto 40.

Matangazo ya kibiashara

Baadhi ya waathirika wa vitendo hivyo walitoka kwenye kijiji cha Kavumu wakiwa na miezi 18 sawa na mwaka mmoja na miezi sita.

Watu hao wanashutumiwa kuwalenga wasichana wadogo kuanzia mwaka 2013 na 2016 kwa sababu za kishirikina wakidaiwa kuwa ni ushauri kutoka kwa waganga wa kienyeji kutumia damu za bikira kwa ajili ya kuwaongezea ulinzi.

Watuhumiwa hao, ikiwa ni pamoja na mbunge Frederic Batumike, na washtakiwa wengine kwa pamoja wamekana mashtaka hayo.

Ni furaha kubwa kwa waathirika na vyama vya kiraia katika kesi ya hii, kesi ambayo ilifunguliwa Novemba 9 katika mkoa wa Kivu Kusini, nchini DRC. Wengi wana matumanini kwamba itapunguza uhalifu na ukatili ambapo wahusika wengi wa ubakaji walikua hawaadhibiwi nchini humo. Washtumiwa kumi na nane, ikiwa ni pamoja na mbunge wa mkoa Frédéric Batumike, wanashtumiwa uhalifu dhidi ya ubinadamu kwa ubakaji wa wasichana arobaini mwaka 2013 na 2016 na kuwa na ushirikiano na kundi la wapiganaji. Siku ya Jumatatu, Novemba 13, mahakama ya kijeshi ilifutilia mbali madai yaliyowasilishwa na upande wa utetezi ili kujaribu kubatilisha utaratibu kwa kusema kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kushughulikia kesi hiyo hiyo, kwa sababu watuhumiwa wote ni raia wa kawaida na mmoja ana kinga ya kutofuatiliwa kutokana na wadhifa wake.

Mahakama ya kijeshi ilithibitisha kwamba ina mamlaka ya kuendelea na kesi hiyo na kuwatuhumu watuhumiwa kumiliki silaha za vita kinyume cha sheria.

Ni mara ya kwanza mbunge kuhukumiwa kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu nchini DRC kwa sababu majaji walitoa uamuzi kuwa mbunge Mbunge Frédéric Batumiké hana kinga dhidi ya mashtaka kwa kiasi kwamba uhalifu unaomkabili unaendana na sheria ya kimataifa.

Zaidi ya watoto arobaini, wenye umri wa miezi 8 hadi miaka 12, walitekwa na kufanyiwa unyanyasaji wa kijinsia kati ya mwezi Mei 2013 na mwaka 2016. Watoto wawili walifariki kutokana na majeraha waliopata.

Mwanzilishi wa hospitali ya Panzi ambayo inasaidia wanawake waliobakwa katika mkoa huo, Denis Mukwege alishtumu mwaka 2014 na 2015 visa hivyo vya utekaji nyara na ubakaji wa wasichana usiku katika kijiji cha Kavumu, karibu mji wa Bukavu.

Kesi hii inatazamia kuendelea Jumanne hii. Wanasheria wa watumiwa, ikiwa ni pamoja na mbunge wa Batumike wameahidi kwamba watakataa rufaa.

Makundi ya haki za binadamu yanamatumaini kuwa, kesi hiyo huenda ikasaidia kumaliza na kukomesha utamaduni wa ubakaji, unaotumika kama nyenzo ya vita nchini DR Congo.