NIGERIA-BOKO HARAM-USALAMA

Nigeria yaendelea kukumbwa na mashambulizi ya kujitoa mhanga

Mji wa Maiduguri unaendelea kukubwa na mashambulizi wa wanamgambo wa Kiislam wa Boko Haram
Mji wa Maiduguri unaendelea kukubwa na mashambulizi wa wanamgambo wa Kiislam wa Boko Haram STRINGER / AFP

Watu wasiopungua 12 waliuawa siku ya Jumatano usiku katika mashambulizi ya kujitoa mhanga yaliyotokea katika mji wa Maiduguri, kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Matangazo ya kibiashara

Mji wa Maiduguri unaendelea kukubwa na mashambulizi ya wanamgambo wa Kiislam wa Boko Haram kwa miaka mnane sasa.

Watu 22 waliojeruhiwa walipelekwa hospitali "ili kutibiwa majeruhi mbalimbali," alisema Bello Dambatta, mkuu wa usalama katika idara ya Usimamizi wa Dharura ya Jimbo la Borno (SEMA).

Washambuliaji wanne wa kujitoa mhanga, wanaume wawili na wanawake wawili, walijipua katika kitongoji cha Muna Garage karibu saa 1:00 usiku za Afrika ya Kati.

Kwa mujibu waBello Dambatta, mshambuliaji wa kwanza alijilipua katikati ya katikati ya waumini wakati wa sala ya jioni, na kuua watu saba. Mshambuliaji mwengine aliingia katika nyumba moja kabla ya kujilipua na kuua mwanamke mmoja mjamzito na mtoto wake. Washambuliaji wengine wawili walijilipua katika mji huo kabla ya kufikia malengo yao, Bw. Dambatta aliongeza.

Kwa upande wake, Victor Isuku, msemaji wa polisi wa jimbo la Borno, alitoa tangazo siku ya Jumatano jioni akisema kuwa milipuko hiyo iligharimu maisha ya watu 14 na kuwajeruhi waengine 29. "Jumla ya watu 18, ikiwa ni pamoja na washambuliaji wanne waliuawa katika milipuko hiyo, wakati ambapo watu 29 waliojeruhiwa walipelekwa kwenye hospitali ya Chuo Kikuu cha Maiduguri," Bw. Isuku alisema.

Vikosi vya usalama vilitumwa haraka "kuhakikisha hali ya kawaida inarejea na "utulivu umerejea katika jamii mbalimbali mjini Maiduguri," alisema.

Nigeria inaendelea kukumbwa na mashambulizi mbalimbali ya Boko Haram.