ZIMBABWE-SIASA-USALAMA

Ujumbe wa Afrika Kusini wakutana na Rais Robert Mugabe

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe wakati wa maadhimisho ya siku ya kuzaliwa kwake Februari 21, 2017.
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe wakati wa maadhimisho ya siku ya kuzaliwa kwake Februari 21, 2017. REUTERS/Philimon Bulawayo

Waziri wa ulinzi wa Afrika Kusini na Waziri wa Usalama wa Taifa, waliotumwa nchini Zimbabwe na Rais Jacob Zuma, ambaye kwa sasa ni rais wa Jumuiya ya nchi za kanda ya kusini mwa Afrika (SADC), wanakutana na Robert Mugabe ikulu," Clayson Monyela, msemaji wa wizara ya Mambo ya Nje ya Afrika Kusini amesema.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe anaamini kuwa bado yuko kiongozi halali wa Zimbabwe na kupinga shinikizo kutoka kwa jeshi linalotaka kumuondoa mamlakani, vyanzo vya siasa na vile vilivyo karibu na idara ya ujasusi vimebaini.

Anashiriki mazungumzo baada ya kuruhusiwa kusafiri hadi kwenye ikulu kutoka makao yake ya kibinafsi ambako amekuwa akizuiliwa na jeshi.

Hata hivyo mpinzani wake wa muda mrefu Morgan Tsvangirai amemtaka ajiuzulu mara moja kwa maslahi ya taifa.

Makamu wa zamani wa Rais Mugabe, Joice Mujuru, pia ametaka kuwe na serikali ya mpito na pia uchaguzi huru na wa kuaminika.

Siku moja baada ya jeshi kuchukua udhibiti wa Zimbabwe, chanzo cha kisiasa kinasema rais Mugabe hana nia ya kujiuzulu kabla ya uchaguzi uliopangwa kufanyika mwaka ujao.

"Ni aina fulani ya mvutano, ni hali tete," kimesema chanzo hicho, ambacho kiliweza kuzungumza na ndugu wa rais Mugabe, ambaye yeye na familia yake wako chini ya kifungo cha nyumbani katika ikulu ya rais mjini Harare.

"Wanasema rais anapaswa kumaliza muhula wake."

Kasisi kutoka kanisa Katoliki, Fidelis Mukonori anajaribu kusuluhisha pande mbili husika katika mvutano huo, ikiwa ni pamoja na rais Mugabe na jeshi, ambalo lilichukua udhibiti wa nchi usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano, likibaini kwamba linawasaka wahalifu walio karibu na Rais Mugabe, mwenye umri wa miaka 93 ambaye yuko madarakani kwa miaka 37.

Majadiliano yanalenga kuunda serikali ya mpito kwa utulivu bila damu kumwagika.

Waziri wa zamani wa Fedha Tendai Biti amesema yuko tayari kujiunga na serikali ya umoja wa kitaifa ikiwa Morgan Tsvangirai atashiriki.