ZIMBABWE-SIASA-USALAMA

Mugabe akataa kuachia mamlaka

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe wakati akihutubia taifa Jumapili, Novemba 19, 2017
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe wakati akihutubia taifa Jumapili, Novemba 19, 2017 STR / AFP

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, katika hotuba yake kwa wananchi wa Zimbabwe siku ya Jumapili, alijizuia kutangaza kujiuzulu, huku akisema kuwa ataongoza mkutano mkuu wa chama wa mwezi ujao.

Matangazo ya kibiashara

Hotuba ya Robert Mugabe iliwashangaza wananchi wengi wa Zaimbabwe, wakati ambapo walikua waisubiri kuwa atatangaza kujiuzulu.

Awali vyanzo vilivyo karibu na washirika wake wa karibu vilibaini kwamba Bw. Mugabe atajiuzu kwa muda wowote, lakini hotub ayake imeonyesha kuwa hana nia ya kujiuzulu.

Siku ya Jumapili mkutano wa dharura wa chama cha Zanu-PF ulimfukuza rais Mugabe kweye uongozi wa chama hicho.

Bw. Mugabe amesema kuwa ataongoza siku zijazo mkutano mkuu wa chama cha Zanu-PF.

"Katika wiki chache, nitaongoza mchakato ambao hautaleta vurugu kwa wananchi wa Zimbabwe. Kwa kumalizia, nataka kusema kuwa najua vizuri sana kuwa kuna maendeleo mengi ndani ya chama, au maendeleo ambayo yanapaswa kufanyika kwa niaba ya chama. Makosa ya zamani na hasira kwa wanachama yanaeleweka kabisa. Hata hivyo, hatuwezi kulipiza kisasi, htunahitajika kuendeleza chama zaidi kuliko na tunahitajika kuwa wanachama bora au Waziimbabwe bora ".

Maafisa wakuu wa chama hicho cha Zanu-PF walikuwa wameidhinisha hatua ya kumvua uongozi wa chama hicho na kumpatia saa 24 ajiuzulu la sivyo wamuondoe madarakani.

Jeshi lilichukua udhibiti wa serikali wiki iliyopita, huku mzozo kuhusu nani atamrithi ukizidi kutokota. Bw Mugabe ameonekana kupoteza udhibiti wa chama chake.

Mzozo wa sasa ulianza Bw Mugabe alipomfuta kazi makamu wake Emmerson Mnangagwa wiki mbili zilizopita, hatua iliyolikera jeshi ambalo lilitazama hatua hiyo kama jaribio la kumteua mke wake Grace kuwa makamu wa rais na mwisho kuwa mrithi wake.

"Bila kujali faida au madhara ya jinsi (jeshi) walitekeleza operesheni yao, mimi, kama amiri jeshi mkuu, nakiri kwamba kuna matatizo," amesema, akirejelea hatua ya jeshi ya kuchukua udhibiti wa runinga ya taifa wiki iliyopita.

Katika mkutano huo pia, Grace Mugabe, 52, alifukuzwa kutoka kwa chama hicho pamoja na maafisa wengine wakuu.