LIBYA-UN-WAHAMIAJI-HAKI

Soko la watumwa Libya: Antonio Guterres alaani

Kwa mujibu wa serikali ya Tripoli, wanawake waliokua walisafiri kupitia bahari wakijaribu kwenda Ulaya, waliokolewa na kikosi cha ulinzi wa mipaka cha Libya, Novemba 6, 2017.
Kwa mujibu wa serikali ya Tripoli, wanawake waliokua walisafiri kupitia bahari wakijaribu kwenda Ulaya, waliokolewa na kikosi cha ulinzi wa mipaka cha Libya, Novemba 6, 2017. REUTERS/Ahmed Jadallah

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amesema kusikitishwa na habari iliyofichuliwa hivi karibuni ya kuwepo kwa soko la watumwa nchini Libya, akisema kitendo hicho kinaweza kuwa uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya taarifa ya kutisha iliyorushwa kwenye kituo cha televisheni cha CNN kuhusu soko la watumwa nchini Libya, viongozi mbalimbali wameendelea kulaani kitendo hicho.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani kitendo hicho, ambacho kimewaathiri wahamiaji kutoka Afrika.

"Ninaogopa na ripoti hizi na video zinazoonyesha wahamiaji wa Afrika wakiouzwa kuwa watumwa nchini Libya," alisema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Ninachukizwa na kitendo hiki cha kutisha na ninatoa wito kwa mamlaka husika kuanzisha uchunguzi, bila kuchelewa, kuhusu kitendo hiki haramu. Pia ninatolea wito mamlaka zote husika kuwafikisha wahusika mbele ya vyombo vya sheria. Niliziomba idara husika katika Umoja wa Mataifa kufanya kazi kikamilifu juu ya suala hili.

"Utumwa hauna nafasi katika ulimwengu wetu"

Utumwa hauna nafasi katika ulimwengu wetu. Vitendo hivini miongoni mwa ukiukwaji wa haki za binadamu ... na vinaweza kuwa uhalifu dhidi ya ubinadamu. Kwa hiyo ninaomba kila taifa kupitisha na kutekeleza Mkataba wa Umoja wa Mataifa dhidi ya Uhalifu wa kimataifa unaoendeshwa... pamoja na itifaki yake kuhusu biashara ya watu. Ninahimiza jumuiya ya kimataifa kuungana kwa kupambana na janga hili, " alisem aAntonio, Guterres.

Viongozi wa Afrika walaani vitendo vya kuuzwa kwa wahamiaji kama watumwa

Rais wa Niger Mahamadou Issoufou, ambaye alielezea masikitiko yake wiki iliyopita, siku ya Jumatatu aliomba Mahakama ya Kimataifa (ICC) "kushughulikia kesi hii" kuuzwa kwa wahamiaji Afrika kama watumwa nchini Libya. Pia aliomba suala hili liwekwa kwenye ajenda ya mkutano kati ya Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya uliopangwa kufanyika tarehe 29 na 30 Novemba mjini Abidjan.

Siku ya Jumapili balozi wa Libya nchini Niger aliitishwa na viongozi wa nchi hiyo kumuelezea hasira ya Rais Issoufou.

Na Burkina Faso imeamua kumuondoa balozi wake nchini Libya kama ishara ya "kuonyesha hasira za serikali ya Burkina Faso na pia kulaani kinachoendelea nchini Libya na kupinga dhidi picha zilizokuepo katika karne zilizotangulia. "