ZIMBABWE-SIASA-USALAMA

Robert Mugabe ajiuzulu kama rais wa Zimbabwe

Rais Robert Mugabe hatimaye ameachia ngazi
Rais Robert Mugabe hatimaye ameachia ngazi REUTERS/Philimon Bulawayo

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, amejiuzulu. Mugabe ametuma barua kwa bunge akisema kuwa anaamua kujiuzulu, kwa mujibu wa spika wa bune la Zimbabwe Jacob Mudenda.  

Matangazo ya kibiashara

Wabune walikua wameaza vikao vya kumtimua madarakani Tangu Jumanne hii. Awali Mkuu wa majeshi, Jenerali Constantino Chiwenga alkizitaka pande husika katika mchakato wa kumuondoa madarakani rais Mugabe kusalia watilivu.

Katika hotuba yake kwenye televisheni, Jenerali Chiwenga alisema ameridhishwa na "maendeleo mapya" tangu mapinduzi ya kijeshi wiki iliyopita, hususan "mawasiliano kati ya rais Mugabe na aliyekua makamu wake Emmerson Mnangagwa, ambaye anatarajiwa hivi karibuni nchini Zimbabwe".

Mkuu wa majeshi ya Zimbabwe, Jenerali Constantino Chiwenga (katikati), Harare, Novemba, 20, 2017.
Mkuu wa majeshi ya Zimbabwe, Jenerali Constantino Chiwenga (katikati), Harare, Novemba, 20, 2017. REUTERS/Philimon Bulawayo

"Sisi, vikosi vya usalama na ulinzi vya Zimbabwe tunawahimiza wananchi wa Zimbabwe kusalia watulivu, na kuheshimu sheria za nchi", pia alisema Jenerali Constantino Chiwenga katika hotuba yake, siku moja kabla ya maandamano mapya dhidi ya Robert Mugabe, madarakani kwa miaka 37.

Jana Jumatatu afisa wa Zanu-PF alisema kuwa hoja ya kumnyang'anya urais itawasilishwa bungeni leo Jumanne na mchakato wa kumng'oa madarakani unaweza kuchukua siku mbili tu.

Mapema Jumanne hii aliyekuwa makamu wa rais Emmerson Mnangagwa alimtaka rais Mugabe kujiuzulu na kukataa kukutana nae kabla hajajiuzu.

Emmerson Mnangagwa, mwenye umri wa miaka 75, aliachishwa kazi tarehe 6 Novemba na kulazimika kukimbilia uhamishoni baada mvutano na mkewe rais Mugabe, Grace Mugabe, mwenye umri wa miaka 52, ambaye alifanikiwa kumuondoa hasimu wake katika kinyang'anyiro cha kumrithi mumewe.

Wananchi wa Zimbabwe sasa wanaandamana katika miji mbalimbali baada ya tangazo hilo la kujiuzulu kwa Robert Mugabe.