Mugabe na viongozi wengine wa afrika walivyoachia ngazi

Kujiuzulu kwa rais Mugabe kwaendeleza historia ya viongozi ving'ang'anizi wa madaraka

Aliyekuwa rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe akisisitiza juu ya msimamo wa serikali yake kuhusu kutaifisha mashamba yaliyokuwa yanamilikiwa na wazungu August 2002
Aliyekuwa rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe akisisitiza juu ya msimamo wa serikali yake kuhusu kutaifisha mashamba yaliyokuwa yanamilikiwa na wazungu August 2002 AFP/STR

Kujiuzulu kwa rais wa Zimbabwe Robert Mugabe alidumu madarakani kwa miaka 37 tangu aingie madakani mwaka 1980 kumeendeleza historia ya viongozi wa afrika waliolazimika kuondoka madarakani baada ya kuhudumu kwa kipindi kirefu.

Matangazo ya kibiashara

February 18 Mwaka 2010 rais wa Niger Mamadou Tandja aliondoka madarakani baada ya kupinduliwa kijeshi akijaribu kubadili katiba ili aendelee kubaki madarakani baada ya kuongoza kwa mihula miwili tangu mwaka 1999.

- 2011 -

Kunako januari 14 mwaka 2011 rais wa Tunisia Zine El Abidine Ben Ali alikumbwa na wimbi la mageuzi na mabadiliko na kulazimika kukimbilia Saudi Arabia akiwa na familia yake.

Mwaka huo huo February 11 rais wa Misri Hosni Mubarak aliondoka madarakani kwa shinikizo la maandamano ya wananchi na kumaliza utawala wake wa miaka 30.

April 11 mwaka 2011 rais wa Ivory Coast aliyekuwa madarakani tangu mwaka 2000 Laurent Gbagbo, alikamatwa baada ya mvutano wa takribani miezi minne akikataa kutambua ushindi wa rais Alassane Ouattara katika uchaguzi wa mwaka 2010.

Oktoba 20 mwaka 2011 ni siku ya kukumbukwa nchini Libya baada ya Dikteta Moamar Gaddafi kukamatwa na kuuawa baada ya kudumu madarakani kwa miaka 42 huku majeshi ya NATO yakisaidia waasi waliokua wakipinga utawala wa Moamar Gaddafi

- 2012 -

March 22, mwaka 2012 serikali ya Mali ikiongozwa na rais Amadou Toumani Toure ilipinduliwa na wanajeshi waasi.

Mwaka huohuo April 12 nchini- GUINEA BISSAU: yalifanyika mapinduzi ya kijeshi na kuondolewa madarakani rais Raimundo Pereira .

- 2013 -

March 24 mwaka 2013 rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Francois Bozize aliondoka madarakani huku makundi ya Seleka na Anti Balaka yakiendelea kukabiliana.

Huko Misri July 3 mwaka 2013 rais Mohamed Morsi, aliondolewa kwa maandamano ya umma baada ya kukaa madarakani mwaka mmoja.

2014 -

October 31 mwaka 2014 rais wa Burkina Faso Blaise Compaore aliondolewa madarakani baada ya kutaka kuendeleza utawala wake akiwa madarakani kwa miaka 27

- 2017 -

January 21 mwaka 2017 rais wa GAMBIA: Yahya Jammeh, alilazimika kukabidhi madaraka kwa Adama Barrow, na kukimbia nchi yake baada ya kukaa madarakani tangu mwaka 1994