Robert Mugabe, rais alieongoza kwa muda mrefu

29 juin 2008. Robert Mugabe est réélu pour un sixième mandat dans un climat tendu et fait face aux critiques internationales.
29 juin 2008. Robert Mugabe est réélu pour un sixième mandat dans un climat tendu et fait face aux critiques internationales. AFP PHOTO / Alexander Joe

Robert Gabriel Mugabe, ambaye alizaliwa tarehe 21 Februari 1924, amekuwa kiongozi wa Zimbabwe tangu 1980 baada ya nchi hiyo kupata uhuru. Pia alikua kiongozi wa chama tawala cha Zanu.

Matangazo ya kibiashara

Mwaka 1980 alikuwa waziri mkuu na mwaka 1987 rais wa Zimbabwe. Kabla ya wakati huo aliongoza upinzani wa Zanu dhidi ya serikali ya walowezi Waingereza nchini Zimbabwe waliofuata siasa ya ubaguzi wa rangi.

Mugabe alichriki katika chaguzi mbalimbali za urais na kuibuka mshindi. Tangu mwaka 2000 chaguzi hizo zilikuwa mashakani kutokana na vitishio na matumizi ya mabavu dhidi ya wapinzani. Utawala wa Mugabe uliitwa wa kidikteta tangu mwaka 2002.

Kutokana na mashataka dhidi ya utawala wa Mugabe ya kudharau haki za binadamu, Zimbabwe ilisimamishwa ndani ya Jumuiya ya Madola. Mugabe pamoja na mawaziri wake na viongozi wa chama chake walipigwa marufuku kusafiri kwenda nchi za Umoja wa Ulaya na Marekani.

Mwanzoni wa utawala wake Mugabe alisifiwa kujenga uchumi na sera ya elimu nchini. Zimbabwe ilikuwa nchi iliyouza vyakula vingi nje. Tangu mwanzo wa milenia mpya pamoja na mashtaka ya udikteta hali ya uchumi ilirudi nyuma. Takriban milioni mbili za raia wa Zimbabwe waliondoka nchini wakikaa kama wakimbizi Afrika Kusini.

Tuhuma za mauaji na ukandamizaji

Baada tu ya kushika madaraka, Mugabe aliamua kuimarisha jeshi lake la kumlinda (liitwalo Gukurahundi) ambalo lilijengwa na watu kutoka kabila lake la wa-Shona. Nchi hiyo ilikuwa tayari imegawanyika kikabila hata katika uchaguzi wa kwanza wa 1980, washona wote walimchagua Mugabe. Wakati ambapo Wa-ndebele walichagua viongozi kutoka chama cha ZAPU kilichoongozwa na Joshua Nkomo.

Mara baada ya uchaguzi tu mwezi Novemba 1980 Mugabe alianza kampeni ya kuua kwa wingi watu wa kabila la Wa-ndebele ambao mji wao mkubwa unaitwa Bulawayo. Ingawa mauaji hayo hayakufikia kiwango cha yale ya Rwanda na Burundi, waliuawa wanawake, wanaume, watoto na hata vichanga vilivyokuwa matumboni. Mwaka 1981 pia Mugabe aliendelea kuua wandebele tukio ambalo halikutangazwa sana na vyombo vya habari. Robert aisi Mugabe alijaribu kushinda kila uchaguzi unaokuja nchini Zimbabwe kwa kutumia nguvu za kikabila na mabavu.

Baada ya uchaguzi wa mwaka 2008, Mugabe alilazimika kugawanya mamlaka na kiongozi wa upinzani Morgan Tsvangirai.

Japo kulikuwa na ghasia dhidi ya wafuasi wa Bw Tsvangirai katika kampeni za uchaguzi

Ndoa yake na Grace Mugabe, anayemzidi kwa maika 40, yaweza kuwa iliyomponza.

Wengi walikasirishwa na Grace kuandaliwa kuwa mrithi wake.

Jeshi limeonesha kumtaka Emmerson Mnangagwa aliyefutwa kazi kama makamu wa Rais na Mugabe mwezi Novemba.

Tarehe 21 Novemba 2017 aliamua kujiuzulu, baada ya shinikizo kutoka chama chake cha Zanu-PF kuomba bunge kuanzisha mchakato wa kumtimua mamlakani. Mugabe aliongoza Zimbabwe kwa miaka 37.