ZIMBABWE-SIASA-USALAMA

Mnangagwa aapishwa na kuchukua hatamu ya uongozi wa Zimbabwe

Rais mpya wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa wakati wa kuapishwa kwake, Harare Novemba 24.
Rais mpya wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa wakati wa kuapishwa kwake, Harare Novemba 24. REUTERS/Mike Hutchings

Hatimaye rais mpya wa Zimbabwe Emmerson ameapishwa rasmi kuchukua wadhifa huo kufuatia kujiuzulu kwa Robert Mugabe siku ya Jumanne wiki hii kwa shinikizo la jeshi na chama chake cha Zanu-PF.

Matangazo ya kibiashara

Mnangagwa ameapishwa kama rais wa Zimbabwe, kufuatia kuondoka kwa rais kuondoka kwa Robert Mugabe madarakani baada ya miaka 37 ya utawala wa kiimla.

“ Mimi Emmerson Dambudzo Mnangagwa naapa kuwa rais wa Zimbabwe. Nitakuwa mwaminifu na kutii na kuilinda Katiba ya nchi,” alisema huku akishangiliwa.

Emmerson Mnangagwa rais mpya wa Zimbabwe akiapishwa jijini Harare
Emmerson Mnangagwa rais mpya wa Zimbabwe akiapishwa jijini Harare REUTERS/Mike Hutchings

Mnangagwa ameshangaliwa na maelfu ya raia wa nchi hiyo waliofika kushuhudia mabadiliko ya uongozini nchini humo.

Amesema kuwa mabadiliko ya umiliki wa ardhi yalifanyika na hayawezi kubadilishwa kwa kuwa huo utakuwa ukiukaji mkubwa wa upiganiaji wa Uhuru.

Lakini rais huo mpya ameahidi kuwalipa wakulima waliopoteza mashamba yao katika sera tata iliotekelezwa na utawala wa rais Mugabe.

''Sina ujuzi wa kazi hii lakini nitawahudumia wananchi wote bila upendeleo wa rangi ama kabila”. Amemsifu Robert Mugabe kwa kupiginia uhuru huku akisema kuwa alichukua uongozi wakati mgumu.

Amesema kuwa licha ya makosa yaliofanywa na Mugabe ni muhimu kukubali na kutambua mchango wake kuhusu ujenzi wa taifa.

Bwana Mnangagwa amesema kuwa amekuwa akiwasiliana na makamanda wakati alipofurushwa na rais Mugabe kama naibu wake.

Alisema kuwa kulikuwa na mpango wa kutaka kumuua ndio sababu akaondoka nchini humo na kurudi siku ya Jumatano baada ya Mugabe kujiuzulu.

Baada ya rais huyo mpya kuapishwa, mizinga 21 ilipigwa kumkribisha rais Emmersonn Mnangagwa.

Umati wa watu ulipiga kelele kufuatia hatua ya jeshi kupiga hewani risasi 21 kama heshima za kumkaribisha rais mpya.

Bw. Mnangagwa aliapa kulinda haki za raia wa Zimbabwe.

Upinzani unamtaka rais Mnangagwa kuwa tofauti na mtangulizi wake na kudumish ademokrasia kwa taifa hilo lililojipatia uhuru wake mwaka 1980.

Mbali na raia wa Zimbabwe, viongozi wengine wa Afrika wanashuhudia mabadiliko hayo akiwemo rais wa Zambia Edgar Lungu na Ian Khama wa Bostwana.

Rais wa zamani Zambia Keneth Kaunda na Rupia Banda nao pia wamehudhuria sherehe hizo jijini Harare.

Emmerson Mnangagwa ataongoza Zimbabwe kwa kipindi cha miezi nane hadi kuelekea uchaguzi mwaka ujao, na tayari chama chake cha Zanu-PF kilimteua hivi karibuni kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi wa urais mwaka ujao.