AFRIKA KUSINI

Pistorius aongozewa kifungo jela na Mahakama ya Juu

Oscar Pistorius
Oscar Pistorius REUTERS/Phill Magakoe/Pool

Mahakama ya Juu  nchini Afrika Kusini imemwongezea kifungo jela mwanariadha mlemavu Oscar Pistorius kwa kosa la kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp bila kukusudia mwaka 2013.

Matangazo ya kibiashara

Pistorius sasa atakitumia kifungo cha miaka 13 jela badala ya miaka sita, adhabu aliyopewa na Mahakama Kuu.

Familia ya Steenkamp inasema haki imetendeka.

Serikali ilikwenda katika Mahakama hiyo kukata rufaa baada ya hukumu ya kwanza, kwa kile kiongozi wa mashtaka alisema hakuridhika na uamuzi wa kwanza.

Viongozi wa mashtaka waliongeza kuwa, mbali na kifungu cha awali Pistorius hakuonesha kujutia kwa namna yeyote ile kuhusu kifo cha mpenzi wake.

Hukumu hii mpya ni pigo kwa Pistorius ambaye ameendelea kukanusha kuwa, alimuua mpenzi wake kwa makusudi kwa kile alichoeleza kwamba alifikiri kuwa alikuwa amevamiwa.