MISRI-UGAI

Zaidi ya watu 54 wauawa katika shambulio dhidi ya Msikiti Sinai, Misri

Mapigano kati ya askari wa Misri na wapiganaji wa kundi la IS kaskazini mwa Sinai, Julai 2, 2015.
Mapigano kati ya askari wa Misri na wapiganaji wa kundi la IS kaskazini mwa Sinai, Julai 2, 2015. AFP/Said Khatib

Zaidi ya watu 54 wameangamia na wengine 75 wamejeruhiwa katika shambulizi la bomudhidi ya Msikiti kaskazini mwa Sinai, chini Misri, kwa mujibu wa shirika la habari la Misri Mena. Shirika hilo, lililonukuu chanzo rasmi, pia limeripoti kuwa kumekuepo na ufyatulianaji risasi katika eneo hilo.

Matangazo ya kibiashara

Shambulio la bomu liliua watu wasiopungua 54 katika Msikiti wa Al Rawdah katika mji wa Bir al-Abed kaskazini mwa Sinai, nchini Misri. Mashahidi wanasema wameona magari ya wagonjwa yakiwabeba hopitalini watu waliojeruhiwa. Idadi ya waliojeruhiwa inaweza kuzidi 75, kwa mujibu wa mashahidi hao.

Rais Abdel Fattah al Sisi ameitisha kikao cha dharura cha usalama, inaripoti televisheni ya serikali imearifu.

Vikosi vya usalama vya Misri vinapambana katika eneo la Sinai dhidi ya kundi la Islamic State (IS). Mamia ya polisi na askari wameuawa katika vita hivyo. Mapigano pia yameongezeka zaidi katika miaka hii mitatu iliyopita.

Magaidi wamekua wakilenga vikosi vya usalama lakini pia Makanisa ya Katoliki ya Misri.