ZIMBABWE-SIASA-USALAMA

Zimbabwe kusherehekea sikukuu ya taifa ya Mugabe

Robert Gabriel Mugabe apewa sikukuu ya taifa nchini Zimbabwe
Robert Gabriel Mugabe apewa sikukuu ya taifa nchini Zimbabwe AFP PHOTO / Alexander Joe

Aliye kuwa rais wa Zimbabwe na mmoja wa waasisi wa uhuru wa Zimbabwe amepwa heshima kubwa nchini humo, baada ya serikali kutangaza leo kwamba Zimbabwe itakua ikisherehekea sikukuu ya taifa ya Robert Gabriel Mugabe.

Matangazo ya kibiashara

Serikali imesema mchango wa Mugabe utakubukwa sana katika jitihada za kupigania uhuru wa nchi hiyo kutoka mikononi mwa Uingereza.

Robert Mugabe aliondolewa mamlakani wiki iliyopita, kufuatia mgongano na uhasama kuhusu nani atakaemrithi kabla ya jeshi kuingilia kati.

Gazeti la serikali la Herald limesema sikukuu hiyo itakuwa ikiadhimishwa siku ya kuzaliwa kwa Bw Mugabe kila mwaka.

Robet Gabriel Mugabe kwa sasa ana umri wa miaka 93, na alizaliwa Februari 21, 1924.

Tangazo hilo lilichapishwa siku ya Ijumaa Novemba 24, siku ambayo Rais Emmerson Mnangagwa alitawazwa kuwa rais mpya wa Zimbabwe, baada ya kutimuliwa kwenye wadhifa wake wa makamu wa rais kufuatia malumbano na mkewe Mugabe, Grace Mugabe.