Maaskofu wamuomba Kabila kutangaza kuwa hatowania katika uchaguzi ujao

Baraza Kuu la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini DRC wamuomba rais kabila kutowania muhula mwengine.
Baraza Kuu la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini DRC wamuomba rais kabila kutowania muhula mwengine. Photo MONUSCO/ John Bompengo

Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wamemtaka rais Joseph Kabila kujitokeza hadharani na kutangaza kuwa hatawnaia urais kwa muhula wa tatu.

Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi Mkuu nchini DRC umepangwa kufanyika nchini humo mwezi Desemba mwaka ujao.

Kauli hii, ya Maaskofu imekuja baada ya mkutano wao kuthamini hali ya kisiasa nchini humo.

Upinzani umekuwa ukidai kuwa rais Kabila, anapanga kuwania tena rais kinyume cha katiba, madai ambayo rais Kabila hajajibu.

 

Yote haya yanakuja wakati huu ambapo Tume ya Uchaguzi imetangaza kuwa Uchaguzi mpya utafanyika tarehe 23 mwezi Desemba mwaka 2018.

Kumekuwa na shinikizo kutoka kwa Jumuiya ya Kimataifa, kwa serikali ya DRC kuhakikisha kuwa Uchaguzi huo unafanyika kama ilivyopangwa.

Hayo yanajiri wakati ambapo serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imepiga marufuku maandamano yaliyopangwa wiki hii kushinikiza kujiuzulu kwa rais Joseph Kabila.

Polisi jijini Kinshasa katika siku zilizopita, wamekuwa wakikabiliana na waandamanaji wa upinzani kwa kuwakamata na hata kuwafwatulia risasi na mabomu ya kutoa machozi.