UFARANSA-AFRIKA-USHIRIKIANO

Macron kuendeleza elimu kwa wasichana wa Afrika

Emmanuel Macron wakati wa hotuba yake Ouagadougou Novemba 28, 2017.
Emmanuel Macron wakati wa hotuba yake Ouagadougou Novemba 28, 2017. REUTERS/Philippe Wojazer

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ambaye ameanza safari yake ya kwanza barani Afrika tangu kuchaguliwa kwake, amewasili nchini Burkina Faso. Rais Macron ametoa hotuba yake mbele ya mamia ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ouagadougou kuhusu sera yake kwa Afrika.

Matangazo ya kibiashara

Rais Macron amewatolea wito vijana wa Afrika kupiga vita ugaidi, biashara haramu ya silaha na biashara ya watu, huku akilaani kile kilichotokea hivi karibuni nchini Libya kuhusu wahamiaji kuuzwa kama watumwa akisema ni hali chafu iliyowakabili wa Afrika katika karne zilizopita.

Rais wa Ufaransa amesema kitendo hicho ni uhalifu dhidi ya binadamu, akiwaomba viongozi wa Afrika kukomesha hali hiyo.

Amewasihi vijana kutopotoshwa na yeyote kwa kujihusisha na ugaidi akisema ni kitendo kibaya ambacho kinahatarisha usalama katika nchi mbalimbali.

Ongezeko la watu ni changamoto kwa Afrika

Rais Macron amesema ongezeko la watu ni changamoto kubwa Afrika. Amesema ni vema nchi za Afrika kukabiliana na ongezeko la watu.

"Ongezeko la watu ni changamoto kwa Afrika na ni jambo ambalo watu mbalimbali wanaweza kukabiliana nayo, " amesema rais Macron.

Ufaransa kuimarisha sekta ya elimu Afrika

Rais wa Ufaransa amewatolea wito viongozi wa afrika kuwasomesha kwa hali na mali vijana, na kuahidi kuwa Ufaransa iko tayari kuendelea elimu hasa kwa wasichana wa Kiafrika, hukua akisema kuwa mamlaka mbalimbali zinazosimamia elimu nchini Ufaransa zitashirikiana na nchi za Afrika katika kuendeleza elimu.

Amewataka vijana kusoma kwa bidii na kuwahimiza wenzao katika hali ya kuiendeleza Afrika. Rais Macron alitoa houtuba yake mbele ya zaidi ya wanafunzi 800 wa Chuo Kikuu cha Ougadougou, hotuba ambayo ilidumu saa moja na dakika arobaini na moja.

Wakati huu rais Macron anajibu maswali ya wanafunzi.