MISRI-USALAMA

Sissi atoa miezi mitatu kwa jeshi kurejesha utulivu Sinai

Abdel Fatah al-Sissi ataka jeshi kurejesha utulivu Sinai.
Abdel Fatah al-Sissi ataka jeshi kurejesha utulivu Sinai. AFP PHOTO / KHALED DESOUKI

Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sissi, leo Jumatano, ametoa miezi mitatu kwa uongozi wa jeshi kuhakikisha usalama umepatikana katika rasi ya Sinai, ambapo mashambulizi yaliyotokea siku ya Ijumaa iliopita yalisababisha vifo vya zaidi ya watu 300.

Matangazo ya kibiashara

"Ni wajibu wenukulinda na kurejea utulivu katika eneo la Sinai ndani ya miezi mitatu ijayo," Bw Sissi amesema katika hotuba alioitoa akiwepo Mkuu mpya wa majeshi.

"Mnaweza kutumia nguvu zote zinazohitajika," amesema rais wa Misri.

mashambulizi dhidi ya msikiti wa al Bir Abed, katika kijiji kilio karibu na mji wa Al Arish katika Sinai Kaskazini, yaliua watu 305 kulingana na ripoti ya mwisho iliyotolewa na mamlaka.

Mashambulizi mabaya kuwahi kutokea katika historia ya hivi karibuni ya Misri. Hakuna kundi ambalo mpaka sasa limedai kuhusika na mashambulizi hayo, lakini ofisi kuu ya mashitaka na mashahidi walisema washambuliaji, ambao walikua zaidi ya thelathini, walikua wakibebelea bendera nyeusi ya kundi la Islamic state (IS).

Umoja wa Kiarabu unapanga kukutana tarehe 5 Desemba, mkutano ambao utajadili mashambulizi hayo, shirika la habari la Misri, Mena, limearifu leo Jumatano.