AFRIKA KUSINI-SIASA

Cyril Ramaphosa kuwania urais Afrika Kusini

Makamu wa rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa .
Makamu wa rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa . REUTERS/Siphiwe Sibeko

Naibu rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa anaelekea kupata uungwaji mkono mkubwa kuelekea mkutano Mkuu wa chama cha ANC, kumpata kiongozi mpya.

Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo utafanyika kati ya tarehe 16 na 20 mwezi huu jijini Johannesburg , na atakayeshinda atawania urais nchini humo mwaka 2019.

Mpinzani wa Ramaphosa ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Nkosazana Dlamini-Zuma.

Mapema mwezi Novemba Makamu wa rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa aliwambia wafuasi wake kuwa uongozi mbaya umeigharimu ANC na uchumi wa nchi hiyo. Aliwataka wafuasi wake kubadilisha hali hiyo katika uchaguzi wa chama.

Hayo yanajri wakati ambapo rais wa Afrika Kusini Jacob zuma anaendelea kukabiliwa na shutma za ufisadi.

Ramaphoza alizaliwa Novemba 17, 1952.