LIBERIA-UCHAGUZI-SIASA

Mahakama Kuu yafutilia mbali madai ya kufutwa kwa duru ya kwanza ya uchaguzi Liberia

Makao makuu ya Wizara ya Sheria Monrovia, ambapo kunapatikana Mahakama Kuu ya Liberia.
Makao makuu ya Wizara ya Sheria Monrovia, ambapo kunapatikana Mahakama Kuu ya Liberia. REUTERS/James Giahyue

Mahakama nchini Liberia imetupilia mbali ombi la kufutwa kwa duru ya kwanza ya uchaguzi mkuu wa rais uliofanywa Octoba 10 iliopita, hivyo kutakuwa na duru ya pili ya uchaguzi ambapo tarehe bado haijawekwa bayana.

Matangazo ya kibiashara

Duru hiyo ya pili itawapambanisha George Weah, mchezaji wa zamani wa soka aliechukuwa nafasi ya kwanza katika duru ya kwanza kwa kujizolea zaidi ya asilia 38 pamoja na Makamu wa rais anaemaliza muda wake Joseph Boakai ambae alipata zaidi ya asilimia 28 katika duru ya kwanza.

Joseph Boakai pamoja na mgombea aliechukuwa nafasi ya tatu kwa asilimia 9.6 ya kura Charles Brumskine wa chama cha Uhuru waliwasilisha kesi mahakamani kuomba kufutwa kwa uchaguzi huo wa duru ya kwanza wakidai umegubikwa na udanganyifu.

Baada ya kusubiri kwa muda mrefu, hatimae jana Alhamisi mahakama ilikata mzizi wa fitna baada ya kusoma kurasa 126 ikionyesha kwamba hapakuwa na udanganyifu mkubwa kama ilivyowakilishwa na wagombea hao wawili.

Kwa mujibu wa jopo la majaji wa mahakama kuu, wagombe hao wawili wameshindwa kuwasilisha ushahidi wa kutosha unaonyesha uwepo mkubwa wa wizi wa kura na hivyo Makahama hiyo imeungana na uamuzi wa tume ya uchaguzi ilioeleza kwamba walalamikaji hawakutoa ushahidi wa kutosha kulingana na wanacho lalamikia.

Hata hivyo mahakama kuu imetoa masharti ya kufanyika kwa duru ya pili, ikiwemo marekebisho ya dafatari la wapiga kura ambalo limekuwa likikosolewa kw kiasi kikubwa.

Muda umeanza kuhesabiliwa kuelekea duru ya pili, Ellen Johnson Sirleaf anamaliza muhula wake mwexzi Januari huku akikoselewa baada ya kutuhumiwa kuwa amefanya makubaliano ya siri na mgombea aliechukuwa nafasi ya kwanza, George Weah, jambo ambalo amekanusha vikali.