AFRIKA KUSINI

ANC yaanza vikao kutafuta mrithi wa Zuma

Rais wa Afrika Kusini na mkuu wa chama cha ANC Jacob Zuma
Rais wa Afrika Kusini na mkuu wa chama cha ANC Jacob Zuma REUTERS/Siphiwe Sibeko

Chama tawala nchini Afrika Kusini ANC kinaanza mkutano wa siku tano kuanzia leo Jumamosi kuchagua kiongozi mpya kika mchuano mkali wa pande mbili ambao unaonekana kama wakati muhimu katika historia ya taifa hilo baada ya ubaguzi wa rangi.

Matangazo ya kibiashara

Mshindi atakaye patikana ataandaliwa kuwa rais ajaye wa nchi hiyo , lakini chama cha ANC kimepoteza umaarufu wake kwa kiasi kikubwa tangu hayati Nelson Mandela alipokiweka madarakani katika uchaguzi wa mwaka wa 1994 ambao uliweka ukomo wa utawala wa wazungu wachache.

 

Rais Jacob Zuma ambaye utawala wake umakumbwa na kashfa za rushwa , atang'atuka madarakani kama kiongozi mkuu wa ANC lakini atasalia kuwa mkuu wa nchi kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2019.

 

Kuongezeka kwa ukosefu wa ajira na serikali ya rushwa vimechangia kuchanganyikiwa miongoni mwa mamilioni ya watu maskini wa Afrika Kusini ambao wanakabiliwa na makao duni na elimu pamoja na kuendelea kwa ubaguzi wa rangi.

 

Wanaowania uongozi wa chama ni mke wa zamani wa rais Zuma, aliyekuwa mkuu wa Umoja wa Afrika Nkosazana Dlamini-Zuma, na Naibu Rais Cyril Ramaphosa, mfanyabiashara tajiri.

 

Mpambano huo unaweza kukigawa chama cha ANC na mkutano huu wa siku tano unatishia kuwa mbaya, na kulazimisha wagombea wote kutoa wito wa mwisho kuhusu umoja.