DRC-UN

Ripoti: Maafisa wa DRC walishiriki mauaji ya wataalamu 2 wa UN Kasai

Bunkonde, l'execution de deux experts ONU
Bunkonde, l'execution de deux experts ONU RFI

Uchunguzi uliofanywa na idhaa ya Radio France International, RFI pamoja na shirika la habari la Reuters umeonesha kuwa maofisa wa Serikali ya DRC walihusika katika kupanga mauaji ya wataalamu wawili wa umoja wa Mataifa kwenye mkoa wa Kasai ya Kati.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti ya RFI na Reuter inaonesha kuwa maofisa wanne wa Serikali ya DRC kutoka idara ya usalama wa taifa walihusika kwenye mauaji hayo, ripoti inayotofautiana na ile iliyotolewa na Serikali ya DRC kueleza kuwa hakukuwa na afisa wa Serikali aliyehusika.

Serikali ya DRC ilidai pia haikuwa inafahamu kuwa wataalamu hao walikuwa kwenye jimbo hilo.

Wataalamu hao Zaida Catalan rais wa Sweden na Mmarekani Michael Sharp waliuwa mwezi Machi wakati walipokuwa wakifanya uchunguzi kuhusi ripoti ya uwepo wa makaburi ya halaiki zaidi ya 40 kwenye mko wa Kasai.

Msemaji wa Serikali ya DRC Lambert Mende amesema Serikali yake inatatizo na tume ya MONUSCO kwa kuwa hawakuwa na taarifa za uwepo wa wataalamu hao kwenye mkoa wa Kasai ya Kati.

Jimbo la Kasai limeshuhudia machafuko tangu kuuawa kwa kiongozi wa kijadi wa eneo hilo Kamuina Nsapu ambaye aliyeuawa mwezi Agosti mwaka uliopita baada ya kumpinga waziwazi rais Joseph Kabila.

Zaidi ya watu elfu 3 wameuawa na wengine zaidi ya milioni 1 na laki 4 wamekimbia makwao, hii ni kwa mujibu wa ripoti ya kanisa katoliki nchini DRC.