ETHIOPIA-HAKI-SIASA

Desalegn atangaza kuwaachilia huru wafungwa wa kisiasa Ethiopia

Waziri mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn.
Waziri mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn. youtube.com

Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn, ametangaza kuwa wafungwa wa kisiasa waliokuwa wakizuiliwa nchini kwa miaka kadhaa katika jela mbalimbali nchini humo wataachiliwa huru, huku akisema kituo cha kuwazuilia wafungwa wa kisiasa pia kitafungwa.

Matangazo ya kibiashara

Bw Hailemariam amesema kituo kikuu cha kuwazuilia wafungwa cha Maekelawi mjini Addis Ababa ambacho HRW tangu 2013 walidai kimekuwa kikitumia mateso kupata habari kutoka kwa washukiwa kitafungwa.

Kituo hicho hatari kimekuwa kikitumiwa kuwatesa watuhumiwa.

Kituo kipya cha kuwazuilia washukiwa kitafunguliwa na kitatimiza viwango vya kimataifa, amesem aWaziri Mkuu wa Ethiopia.

Pia amesema mashtaka dhidi ya watuhumiwa ambao kesi zao bado hazijamalizika yatafutwa.

“Tunafanya hivyo ili kutoa fursa ya kuwepo kwa mashauriano ya kisiasa, “ amesea Waziri Mkuu wa Ethiopia katika mkutano na waandishi wa habari.

Ni mara ya kwanza kwa serikali ya Ethiopia kukiri kwamba inawashikilia wafungwa wa kisiasa. Awali ilikua ikiwaita “wahalifu”.

Wanaharakati wa haki za binadamu wanasema hatua hii huenda ikaatoa sura mpya kwa haki za binadamu nchini Ethiopia.

Shirika la kimataifa la Hakiki za Binadamu la Human Rights Watch limekuwa likiituhumu Ethiopia kutumia sheria za kukabiliana na ugaidi kuwafunga wapinzani wake.