AFRIKA KUSINI-AJALI

Ajali ya treni yaua watu 14 nchini Afrika Kusini

Mji wa Johannesburg, karibu na eneo kulikotokea  ajali ya treni iliyoua watu wasiopungua 14.
Mji wa Johannesburg, karibu na eneo kulikotokea ajali ya treni iliyoua watu wasiopungua 14. ©Grabowsky/Photothek via Getty Images

Watu wasiopungua kumi na nne wamefariki dunia katika ajali iliyotokea leo Alhamisi nchini Afrika Kusini. Zaidi ya Watu arobaini wamejeruhiwa, kwa mujibu wa idara ya huduma za dharura.

Matangazo ya kibiashara

Ajali hiyo ilitokea kwenye barabara inayounganisha Port- Elizabeth na Johannesburg, Shirika la Reli la Afrika Kusini limebaini.

Awali, maafisa wa huduma za dharura waliripoti kuwa watu nne ndio walipoteza maisha na wengine wengi walijeruhiwa, lakini msemaji wa kampuni ya Shosholoza Meyl amesem awatu kumi nne ndio wamefariki dunia katika ajali hiyo.

Kwa muijbu wa mashahidi wakinukuliwa na shirika la habari la Reuters, treni ilitoka kwenye barabara yake na kugonga lori kabla ya kuwaka moto, karibu na mji wa Kroonstad, katikati mwa Afrika Kusini, kilomita 200 kusini magharibi mwa Johannesbourg.

Ajali hii imetokea wakati wa likizo kuu ya shule nchini Afrika Kusini.