DRC-MAFURIKO

Mafuriko yasababisha watu 37 kupoteza maisha jijini Kinshasa

Mafuriko jijini Kinshasa Januari 04 2018
Mafuriko jijini Kinshasa Januari 04 2018 /www.radiookapi.net

Watu 37 wamepoteza maisha jijini Kinshasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya mvua kubwa kusababisha mafuriko makubwa katika mitaa kadhaa ya jiji hilo.

Matangazo ya kibiashara

Wizara ya afya nchini humo inasema watu walioathirika ni wale wanaoishi katika mitaa duni hasa ule wa Ngaliema.

Kati ya watoto wawili au watatu, ni miongoni mwa watu waliopoteza maisha kutokana na mafuriko hayo huku mamia wakisalia bila makaazi.

Jiji la Kinshasa limeendelea kukabiliwa na mafuriko mara kwa mara mvua inaponyesha kutokana na miundo mbinu mibaya hasa mitaro ya kupitsiha maji na msongamano wa makaazi ya watu.

Maakazi mengi ya watu yamejengwa katika maeneo ya milima, katika eneo hilo lenye watu Milioni 10.