DRC-MONUSCO-SIASA-USALAMA

Chama tawala DRC chaishtumu Monusco kutotekeleza majukumu yake

Msafara wa magaji ya kijeshi ya Monusco, DRC.
Msafara wa magaji ya kijeshi ya Monusco, DRC. CC/MONUSCO/Clara Padovan

Chama tawala nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo PPRD kinaituhumu tume ya kulinda amani nchini humo MONUSCO kwa kuingilia mambo ya kisiasa na kuacha kutekeleza majukumu yake.

Matangazo ya kibiashara

Kauli ya chama hichi imekuja siku moja tu baada ya baraza la usalama la umoja wa Mataifa kuitaka Serikali kuunda tume ya uchunguzi kubaini waliohusika na unyanyasaji dhidi ya waandamanaji na kuvamia makanisa mwisho wa mwaka uliopita.

Katibu mkuu wa chama hicho Henry Mova Sakani, amesema anashangazwa na matamshi ya umoja wa Mataifa aliyosema ni upotoshaji na kuutaka kutoingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo.

Juma moja lililopita watu zaidi ya 7 walipoteza maisha katika maandamano yaliyoitishwa na kanisa katoliki kupinga utawala wa rais Kabila, maandamano ambayo vyombo vya usalama vinalaumiwa na umoja wa Mataifa kwa kutumia nguvu kupita kiasi kudhibiti maandamano.