EQUATORIAL GUINEA-USALAMA

Equatorial Guinea : Jaribio la mapinduzi lilipangwa nchini Ufaransa

Teodoro Obiang Nguema Mbasogo, rais wa Equatorial Guinea.
Teodoro Obiang Nguema Mbasogo, rais wa Equatorial Guinea. AFP/Emmanuel Dunand

Nchi ya Equatorial Guinea imesema kuwa jaribio la mapinduzi dhidi ya serikali yake lilipangwa nchini Ufaransa nchi hiyo ikipaza sauti yake kuwa raia wake wanaoishi barani Ulaya walihusika.

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na waadishi wa habari, Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Equatorial Guinea Agapito Mba Makuy amesema jaribio hili halina uhusiano wowote na Serikali ya Ufaransa na kwamba watashirikiana na nchi hiyo pindi watakapopata taarifa kamili.

Mokuy amesema kuwa kutokana na jaribio hili nchi yake imesitisha utolewaji wa bure wa visa za kuingia nchini humo kwa raia kutoka mataifa sita ya Afrika ya kati na Magharibi.

Serikali inasema mamluki 27 wamekamatwa na vyombo vya dola na wengine zaidi ya 150 wanasakwa kwenye eneo la mpaka wa nchi hiyo na Cameroon.

Nchi ya Equatorial Guinea imekuwa ikiongozwa na familia ya Teodoro Obiang Nguema toka mwaka 1979.