COTE D'IVOIRE-HAKI

Mshirika wa karibu wa Gbagbo ahukumiwa miaka 10 jela

Mejat Jean-Noël Abehi, msaidizi wa karibu wa rais wa zamani wa Cote d'Ivoire Laurent Gbagbo.
Mejat Jean-Noël Abehi, msaidizi wa karibu wa rais wa zamani wa Cote d'Ivoire Laurent Gbagbo. AFP PHOTO/ SIA KAMBOU

Msaidizi wa karibu wa rais wa zamani wa Cote d'Ivoire Laurent Gbagbo, aliyeondolewa madarakani mwaka 2011, amehukumiwa jela miaka 10.

Matangazo ya kibiashara

Meja Jean-Noel Abehi amepwewa adhabu hiyo baada ya kupatikana na kosa kujaribu kumwondoa madarakani rais wa sasa Allasane Outtara.

Mahakama jijini Abidjan imesema Abehi, katika mipango yake, alikuwa na vikao katika nchi jirani ta Ghana akiwa amevalia sare za kijeshi akishirikiana na msemaji wa zamani wa Gbagbo, Kone Katinan,kujaribu kuipindua serikali.

Wakati wa utawala wa Ghabgo, Abehi alikuwa Kamanda katika kambi ya askari wa wanajeshi jijini Abidjan.

Mbali na Abehi, washirika wengine wa Gbagbo ambao anazuiliwa katika Mahakama ya ICC ambao wamehukumiwa nchini Cote d'Ivoire ni pamoja na waziri wa zamani Hubert Oulaye ambaye amehukumiwa jela miaka 20.