Pata taarifa kuu
ANGOLA-VYOMBO VYA HABARI

Radio Ecclesia yaruhusiwa kupeperusha matangazo yake Angola

Joao Lourenço, Februari 3, 2017 Luanda, Angola.
Joao Lourenço, Februari 3, 2017 Luanda, Angola. AMPE ROGERIO / AFP
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Kanisa Katoliki nchini Angola wamekaribisha hatua ya rais wa nchi hiyo Joao Lourenço kuruhusu Radio Ecclesia inayomilikiwa na kanisa Katoliki kurusha matangazo yake nchini kote Angola. Kwa sasa, Radio Ecclesia inaweza tu kurusha matangazo yake katika mji mkuu pekee.

Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huu unaonyesha uhusiano kati ya serikali ya Luanda na kanisa Katoliki, ambalo wakati mwingine limekuwa likionekana kama mkosoaji mkubwa wa utawala.

Ujumbe huo umefurahisha waumini wa Kanisa Katoliki wakati wa mkutano wa kwanza wa rais Joao Lourenço na waandishi wa habari mapema wiki hii mjini Luanda. Radio Ecclesia itaruhusiwa kurusha matangazo yake nchini Angola, si tu katika mji mkuu. "Hii ni redio ya kanisa ambayo tunaona kuwa inajiheshimu," Rais wa Angola amesema. Kupanua matangazo ya radio hii itatusaidia sana, labda, kuzuia kuenea kwa makundi ya itikadi yaliyoonekana nchini kwetu katika miaka ya hivi karibuni. "

Kwa upande wa msemaji wa Baraza kuu la Maaskofu nchini Angola, Askofu José Manuel Imbaba, huu ni mwisho wa "kuminywa kwa haki". "Nakaribisha uamuzi wa rais wa Jamhuri na kumshukuru kwa ujasiri wake wa kisiasa," Askofu Imbaba amesema. Sasa ni juu yetu kuinua juhudi zetu na kufanya jambo sahihi ili sauti ya kanisa isikike nchini kote. "

Kuiruhusu Radio Ecclesia ni muhimu sana wakati ambapo Kanisa limekuwa likionekana, kama mkosoaji mkubwa wa utawala. Maaskofu tayari wameunga mkono, katika barua yao, kwamba Waangola wangeweza tu kuwa na"ndoto", miaka 40 baada ya uhuru, nchi yao "kustawi, kujiendeleza kidemokrasia na rushwa kupigwa marufuku".

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.