UGANDA-DRC-UN-USALAMA

Rais Museveni: Umoja wa Mataifa unalinda magaidi DRC

Rais wa Uganda Yoweri Museveni katika moja ya makazi yake Rwakitura, magharibi mwa Uganda mnamo Februari 21, 2016.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni katika moja ya makazi yake Rwakitura, magharibi mwa Uganda mnamo Februari 21, 2016. REUTERS/James Akena

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amelishtumu jeshi la kulinda amani la Umoja wa Mataifa nchini DRC MONUSCO kwa kuwalinda magaidi nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Museveni amesema jeshi la la Umoja wa Mataifa nchini DRC (MONUSCO) limeshindwa kupambana na waasi wa ADF NALU ambao amewaalezea kuwa magaidi.

Tuhma hizi nzito zimetolewa na rais Museveni baada ya kukutana na viongozi wa umoja wa Mataifa wanaochunguza vifo vya wanajeshi 15 wa Umoja wa Mataifa vilivyotokea mwaka uliopita.

"Umoja wa Mataifa unahusika na kulinda magaidi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo," Museveni ameiambia wachunguzi wa Umoja wa Mataifa, kulingana na taarifa kutoka ofisi yake.

Museveni hakutoa maelezo zaidi kuhusu tuhuma hizo na msemaji wake hakujibu wito uliomtaka kutoa maelezo. Mpaka sasa Umoja wa Mataifa haujajieleza kuhusu tuhuma hizo nzito.