DRC-SIASA-MAANDAMANO-CENCO

Polisi watumia nguvu kuzuia maandamano dhidi ya rais Kabila nchini DRC

Maandamano yalivyokuwa jijini Kinshasa Januari 21 2018
Maandamano yalivyokuwa jijini Kinshasa Januari 21 2018 JOHN WESSELS / AFP

Polisi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo walikabiliana na waandamanaji siku ya Jumapili, kumshinikiza rais Joseph Kabila kuondoka madarakani kuelekea Uchaguzi Mkuu mwezi Desemba mwaka huu.

Matangazo ya kibiashara

Polisi walitumia mabomu ya machozi na risasi za moto kuwasambaratisha waandamanaji waliokuwa wamemaliza ibada ya siku ya Jumapili tayari kuanza maandamano.

Maandamano haya yalipangwa na Kanisa Katoliki, ambalo linamtaka rais Kabila kuheshimu makubaliano ya kisiasa ya mwezi Desemba mwaka 2016.

Mwandishi wa RFI Kiswahili jijini Kinshasa Emmanuela Zandi, ameripoti kuwa allishuhudia miili ya waandamanaji 10 waliopigwa risasi na kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa.

"Nimeshuhudia waandamanaji 10 waliopoteza maisha, sehemu iliyokuwa hapa jijini Kinshasa,"

"Viongozi wa Kanisa Katoliki wamekasirika sana na kusema maandamano mengine yatafanyika Jumapili ijayo," aliongeza Zandi.

Mahojiano na Mwandishi wetu wa Kinshasa Emmanuel Zandi kuhusu maandamano dhidi ya rais Joseph Kabila

Serikali kuanzia siku ya Jumamosi, ilizima mtandao wa Internet kwa lengo la kuzuia mawasiliano kupitia facebook, twitter na Whatsapp.

Serikali nchini DRC kupitia jeshi la Polisi, imesema haitaruhusu maandamano hayo kwa kile wanachosema inaharibu usalama wa nchi hiyo.