LIBERIA-SIASA

George Weah kuapishwa rais mpya wa Liberia

George Weah anaapishwa kuwa rais mpya wa Liberia, baada ya kushinda Uchaguzi wa urais mwaka uliopita.

Rais mpya wa Liberia George Weah
Rais mpya wa Liberia George Weah REUTERS/Thierry Gouegnon
Matangazo ya kibiashara

Maelfu ya raia wa Liberia wakiwemo marais kadhaa hasa kutoka Afrika Magharibi wanahudhuria sherehe hizo zitakazofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Monrovia.

Mbali na viongozi wa mataifa ya Afrika, wachezaji wa mchezo wa soka kama Didier Drogba na Samwel Eto'o miongoni mwa wengine watahudhuria sherehe hiyo.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, mchezaji huyo zamani wa mchezo wa soka, alisema kazi yake kubwa itakuwa ni kuhimiza amani nchini humo.

Kuapishwa kwa Weah kunamaliza, uongozi wa rais Ellen Johnson Sirleaf ambaye amekuwa akiongoza nchi hiyo tangu mwaka 2006.

Bi.Sirleaf anaondoka akiwa na rekodi nzuri ya kuhimiza amani nchini humo baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.