DRC-USALAMA-SIASA

DRC yaendelea kuwashikilia watu walioshiriki maandamano

Polisi ikiwakamata baadhi ya waandamanajii, Januari 21, 2018.
Polisi ikiwakamata baadhi ya waandamanajii, Januari 21, 2018. REUTERS/Kenny Katombe TPX IMAGES OF THE DAY

Wanafunzi wa chuo kikuu cha jijini Kinshasa waliandamana jana kupinga kufukuzwa chuoni kwa wenzao wanaotuhumiwa kushiriki katika maandamano ya upinzani ya Novemba mwaka jana kumtaka rais Joseph Kabila kujiuzulu.

Matangazo ya kibiashara

Aidha, Wanafunzi hao wanapinga ongezeko la ada inayotozwa ili kujiunga na chuo hicho.

Mbali na hilo, wananchi wamevilaumu vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa kushindwa kuwalinda raia wakati wa maandamano.

Mkurugenzi wa ofisi ya haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Abdul Aziz Choy amesema wanaendelea kushiirikiana na serikali kufahamu idadi ya waliopoteza maisha.

Hivi karibuni Ubelgiji ilizitaka nchi za Ulaya na Marekani kuichukulia hatua kali serikali ya DRC kwa kuminya uhuru wa kuandamana na kuvunja haki za binadamu.

Watu kadhaa walipoteza maisha katika maandamano hayo na wengine wengi wanaendelea kukamatwa.