NIGERIA-USALAMA

Shambulio la Bomu laua watu wanne Nigeria

Wanajeshi wa Nigeria wakijianda kupiga doria usiku katika msitu wa Sambisa, katika eneo linalodhibitiwa na Boko Haram (Aprili 2014).
Wanajeshi wa Nigeria wakijianda kupiga doria usiku katika msitu wa Sambisa, katika eneo linalodhibitiwa na Boko Haram (Aprili 2014). © RFI/Ben Shemang

Watu wanne wamepoteza maisha katika shambulio la kujitowa muhanga katika kambi ya wakimbizi ilioko mjini Maiduguri Kaskazini mashariki mwa Nigeria, kundi la Boko Haram linashukiwa kuhuska na shambulio hilo.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa zinaeleza kuwa mshambuliaji aliruka ukuta wa kambi ya Dolari na kulipua bomu baada ya kujicahnganya miognoni mwa wakimbizi kambini humo na kuwauwa watu wanne huku wengine 44 wakijeruhiwa baadhi wakiwa katika hali mbaya.

Licha ya kuwa hakuna kundi lililojigamba kuhusika, kundi la Boko Haram linashukiwa kuwa ndilo limehusika na shambulio hilo.

Muda mfupi baada ya hapo mshambuliaji mwingine wa kike alijilipua bila hata hivyo kusababisha madhara yoyote.

Taarifa zinaeleza kuwa mwanamke mmoja aliejichanganya miongoni mwa watu kambini hapo, lakini baada ya kushukiwa, watu wote walimkimbia kabla ya kujilipua.

Mashambulizi hayo yanakuja wakati huu makundi ya wapiganaji wajadi wakijiandaa kukabiliana na wapignaji wa kijihadi wa Boko Haram kuwaondoa katika msitu wa Sambisa.