AFRIKA KUSINI-MAJANGA ASILI

Afrika Kusini: Mji wa Cape Town kukabiliwa na ukame

Mji wa Cape Town, Afrika Kusini.
Mji wa Cape Town, Afrika Kusini. CC/Pixabay/sharonang

Mji wa Cape Town nchini Afrika Kusini unakabiliwa na ukame mkubwa ambao unaweza kusababisha wakazi wa mji huo kukosa maji ya kutumia.

Matangazo ya kibiashara

Mji huu unaotembelewa na watalii wengi kutoka mataifa mbalimbali unajiandaa kuingia katika siku mbaya "Day Zero, wakati hifadhi ya maji itakuwa katika kiwango cha chini sana (13.5% dhidi ya 26% kwa sasa), na hali hiyo itasababisha uhaba wa maji katika mji huo.

Wanasayansi wanatabiri kuwa "Day Zero" itatokea katikati ya mwezi Aprili.

Wakati wakisubiri mvua, wakazi wa Cape Town wanalazimika kuhifadhi maji mengi. iku ya Alhamisi, Februari 1, sheria mpya ilianza kutumika: Kwa sasa, matumizi ya maji ya bomba yamepangwa hadi lita 50 kwa siku na kwa mtu mmoja, vinginevyo wakazi wanaweza kukabiliwa na faini kubwa.

Mwandishi wa RFI alitembelea kwenye mojawapo ya vyanzo vya maji kutoka mlimani mjini Cape Town, ambako wananchi wanakuja kuteka maji kwa bure ili kuepuka kufungua mabomba yao.

Chanzo cha maji cha Newlands kinapatikana mbali na mji

huku kukiwa na mteremko wa mlima wa Jedwali. Tangu mwezi mmoja uliopita, mamia ya watu wanakuja mchana na usiku kuteka maji kwa minajili kuyahifadhi ili kuepuka faini.