DRC-USALAMA

DRC: John Tshibangu atarejeshwa kutoka Tanzania

Rais Kabila anaendelea kukabiliwa na upinzani mkali kutokana na nia yake ya kutaka kugombea urais kwa muhula wa tatu baada ya muhula wake wapili kumalizika mwezi Disemba 2016.
Rais Kabila anaendelea kukabiliwa na upinzani mkali kutokana na nia yake ya kutaka kugombea urais kwa muhula wa tatu baada ya muhula wake wapili kumalizika mwezi Disemba 2016. JOHN WESSELS / AFP

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yimethibitisha kuwa Kanali wa zamani wa jeshi la nchi hiyo John Tshibangu atarejeshwa kutoka Tanzania baada ya kukamatwa siku ya Jumatatu wiki hii.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, mamlaka nchini Tanzania zimemkamata Kanali wa Jeshi la DRC, John Tshibangu aliyetishia kumpindua Rais Kabila baada ya siku 45. Taarifa hiyo imeeleza kuwa, Tshibangu alikamatwa katika uwanja wa ndege Dar es Salaam,

Rais Kabila alimaliza muhula wake wa pili na wa mwisho kikatiba kuwa Rais mwezi Disemba 2016 lakini hajaachia madaraka, mengi yamesemwa na Serikali ikiwemo “hatuna pesa za kutosha kufanya Uchaguzi Mkuu”.

January 19, 2018 Kanali John Tshibangu aliasi na kutangaza vita dhidi ya Rais Kabila, huku akiimpa siku 45 aachie madaraka.

Asubuhi ya Ijumaa January 19 2018 Wanajeshi walionekana kuizingira kwa wingi Ikulu ya Kinshasa huku video iliyorekodiwa na Kanali Tshibangu ikiendelea kusambaa ambapo ndani yake alionekana kazingirwa na Wanajeshi wenye silaha.

Kwenye video hiyo Tshibangu alinukuliwa akisema “Nafahamu siri ya Rais Kabila, sasa ni muda wa kuondoa Serikali ya Mabeberu na Udikteta, na ni lazima Rais Kabila aombe msamaha kwa Wakongo kuanzia Makanisani, Shuleni na hata Raia wa kawaida kwa kosa la kushindwa kuiongoza nchi”.

“Mimi kama Mwananchi mwenye msimamo na huruma kwa mateso yenu, niliamua kujitokeza ili kumfukuza Joseph Kabila kwa nguvu za vita na kijeshi, nawahakikishia kwamba tutamuwinda na atakimbia, ” alisema John Tshibangu.

Tshibangu alilitaja kundi lake la Waasi kwamba linaitwa “Forces Nouvelles du Congo” ikimaanisha Nguvu Mpya kwa Ajili ya Congo.

Rais Kabila anaendelea kukabiliwa na upinzani mkali kutokana na nia yake ya kutaka kugombea Urais kwa muhula wa tatu baada ya muhula wake wapili kumalizika mwezi Disemba 2016.