SENEGAL-UFARANSA-ELIMU

Mkutano mkuu kuhusu elimu kuzinduliwa Dakar, Senegal

Emmanuel Macron na Macky Sall, Februari 2, 2018 Dakar.
Emmanuel Macron na Macky Sall, Februari 2, 2018 Dakar. REUTERS/Ludovic Marin/Pool

Mkutano mkuu kuhusu kufadhili elimu unafanyika leo Ijumaa katika mji mkuu wa Senegal, Dakar. Mkutano huu utaongozwa na rais wa Senegal Macky Sall na mgeni wake wa heshima rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ambaye anaanza ziara ya kiserikali nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Nchi sitini na tano zinazoendelea zinanufaika na mfuko huu. Lengo ni kuuongeza dola bilioni 3. Kwa kuzingatia ahadi zilizotangazwa Ouagadougou mnamo mwezi Novemba, Emmanuel Macron sasa anajaribu kuzitekeleza kwa vitendo.

Kuifanya Senegal, kama Tunisia, maabara ya elimu, kuanzia shule ya msingi hadi elimu ya juu. Katika maono ya rais Emmanuel Macron, elimu, kipaumbele nchini Ufaransa lazima pia iwe ni kipaumbele barani Afrika.

Kwa ushirikiano na mwenyeji wake Macky Sall, rais wa Ufaransa atazindua mradi wa ujenzi wa kwanza wa shule 17 zitakazojengwa mjini Dakar, kisha kutangaza kuundwa kwa chuo kikuu kitakachomilikiwa na Senegal na Ufaransa, chuo kitakachojihusisha na masuala ya sayansi. Chuo Kikuu hiki kinaanzishwa kwa jitihada za rais wa Senegal, ambaye amekua akisema kunahitajika barani Afrika mafundi zaidi na wahandisi. Rais Macky Sall amesema wanafunzi wanapaswa kupewa mafunzo ya kutosha barani Afrika kisha kuwasafirisha nje kuendelea na taaluma yao.

Wadau wote watakaoshiriki mkutano huoWashiriki wote wanakubaliana kuwa elimu inafadhiliwa katika nchi zinazoendelea. Viongozi wengi kutoka Arika wanatarajia kuhudhuria mkutano huo hasa viongozi kutoka Mali, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Togo, Burkina, waruhusu kuongezwa kwafedha, zaidi ya dola bilioni 3 zinahitajika , na Ufaransa inaweza kuchangia hadi 10%. Kiwango kikubwa cha fedha, lakini ambacho kitasaidia tu miradi ya miaka 2018-2020.