GUINEA-SIASA

Hatimaye Uchaguzi wa serikali za mitaa wafanyika nchini Guinea

Raia wa Guinea wakati wa kampeni za mwisho kabla ya kupiga kura Jumapili Februari 04 2018
Raia wa Guinea wakati wa kampeni za mwisho kabla ya kupiga kura Jumapili Februari 04 2018 www.rfi.fr/afrique

Raia wa Guinea wanapiga kura siku ya Jumapili  kuwachagua viongozi wa serikali za mitaa, baada ya uchaguzi huo kuahirishwa kwa muda wa miaka minane.

Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi huu ulikuwa umpangwa kufanyika mwaka 2010 lakini umekuwa ukiahirishwa kwa sababu mbalimbali hasa mzozo wa kisiasa nchini humo.

Tume ya Uchaguzi imesema wapiga kura Milioni 5.9 wanashiriki katika zoezi hili la kihistoria.

Wanasiasa mbalimbali wamekuwa wakitoa ahadi, ikiwemo kuunda nafasi ya ajira, kuimarisha usalama miongoni mwa mambo mengine mengi.

Uchaguzi huu utashuhudia kuchaguliwa kwa Mameya wa miji mbalimbali.