ISRAEL-WAHAMIAJI-USALAMA

Israel kuwatimua wahamiaji wa Afrika

Polisi ya Israel yafanya msako kwa wahamiaji wa Kiafrika katika mitaa ya Tel Aviv, Juni 11, 2012.
Polisi ya Israel yafanya msako kwa wahamiaji wa Kiafrika katika mitaa ya Tel Aviv, Juni 11, 2012.

Mamlaka ya Israeli jana siku ya Jumapili ilianza kusambaza barua kwa maelfu ya wahamiaji wa Afrika, wanaoishi kinyume cha sheria nchini humo kuwataka kuondoka hadi kufikia mwisho wa mwezi ujao.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa idara ya uhamiaji ya Israel ameliambia shirika la habari ya ufaransa AFP kuwa ambao watakaidi amri hiyo watakamatwa na kufungwa gerezani.

Mapema mwezi Januari Waziri Mkuu wa nchi hiyo Benjamin Netanyahu alitangaza kuanzishwa kwa mpango wa kuwaondowa wahamiaji haramu wapatao thelathini na nane elfu, wengi wao kutoka Eritrea na Sudan.

Mapema mwezi Januari Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema Wahamiaji wa Kiafrika watafungwa jela ikiwa hawataondoka Israeli ikifikia tarehe iliyopangwa kuwa wawe wameshaondoka.

Hivi karibuni serikali ya Israel ilitangaza nia yake ya kulipa dola 3,500 (sawa na euro 2,900) kwa wahamiaji kutoka Afrika wanaoishi kinyume cha sheria nchini humo ili kuwahimiza kuondoka Israeli ifikapo mwishoni mwa mwezi Machi, muda ambao watakabiliwa na kifungo ikiwa watakamtwa.

Wengi wa wahamiaji wa Afrika wanatoka Eritrea na Sudan. Wengi wanasema wamekimbia vita, matatizo mbalimbali ya kiuchumi na mateso, lakini Israeli inawachukulia kama wahamiaji "wa kiuchumi".

Mbali na kupewa kitita cha dola 3,500, wahamiaji watalipiwa nauli ya ndege kurudi nyumbani, au kuelekea "nchi nyingine". Nchi ambazo zimekubali kuwapokea ni Rwanda na Uganda, kulingana na mashirika ya haki za binadamu.

"Tumefukuza wahamiaji haramu 20,000 na sasa lengo letu ni kuwafukuza wengine," Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu alisema katika kiako cha baraza la mawaziri katika kuidhinisha mpango huo.

Aliongeza kuwa kizuizi kilichojengwa kando ya mpaka na Misri kimezuia wakimbizi wengi kutoka Afrika. Alielezea tatizo la usalama kwa Waisraeli wanaoishi katika vitongoji maskini kusini mwa Tel Aviv ambapo wahamiaji wengi kutoka Afrika wanaishi.

Kwa mujibu wa afisa wa uhamiaji ambaye hakutaka jina lake litajwe, wahamiaji 38,000 wanaishi kinyume cha sheria nchini Israel na zaidi ya 1,400 wanafungwa katika vituo viwili.

Wahamiaji, ambao baadhi yao wamekuwa wakiishi Israeli kwa miaka mingi, wana kazi lakini wanalipwa vibaya, kazi ambazo Waisraeli hawataki..

Benjamin Netanyahu alisema kuwa uwepo wa wahamiaji nchini Israel ni tishio kwa Waisrael.