DRC-USALAMA

Kiongozi wa kundi la waasi ajisalimisha kwa vyombo vya usalama DRC

Wakimbizi wa ndani wa Kasaï wakisubiri chakula cha siku katika kambi ya Kikwit, Juni 3, 2017.
Wakimbizi wa ndani wa Kasaï wakisubiri chakula cha siku katika kambi ya Kikwit, Juni 3, 2017. JOHN WESSELS / AFP

Kiongozi mmoja wa kundi la wapiganaji anayedaiwa kuongoza mauaji kwenye mkoa wa Kasai nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, amejisalimisha mwenyewe kwa mujibu wa vyombo vya usalama nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa kiongozi wa eneo la Mweka mkoani Kasai Jacopo Pembe Longo, amethibitisha kujisalimisha kwa kiongozi wa kijadi Chifu Kalamba Dilondo aliyejisalimisha kwa hiari yake kwenye kituo cha Kakenge.

Longo amesema kuwa baada ya kujisalimisha kwa Dilondo aliyepokelewa na gavana wa jimbo hilo, alikabidhiwa kwa vyombo vya usalama tayari kwa kuchukuliwa hatua za kisheria kutokana na kuhusika kwake kwenye mauji ya raia mkoani Kasai.

Mkoa wa Kasai umetumbukia kwenye machafuko tangu mwezi September mwaka 2016 mwezi mmoja tu baada ya vyombo vya usalama kumuua aliyekuwa kiongozi wa kijadi kwenye mkoa huo Kamwina Nsapu.

Tarehe 30 Januari mwaka huu watu 9 waliuawa baada ya wapiganaji wanaodaiwa kuwa wa Kamwina Nsapu kwenda kuwasaidia wapiganaji wa Kalamba na kuchoma moto mamia ya nyumba.