DRC-UN-USALAMA-HAKI

Umoja wa Mataifa wataka haki itendeke kwa kesi ya Tshimbangu

Waziri wa Sheria na Haki za Binadamu wa DRC, Alexis Tambwe Mwamba (kulia) akizungumza na Mkurugenzi wa UNJHRO, José Maria Aranaz.
Waziri wa Sheria na Haki za Binadamu wa DRC, Alexis Tambwe Mwamba (kulia) akizungumza na Mkurugenzi wa UNJHRO, José Maria Aranaz. Photo MONUSCO/Daniel Wangisha

Tume ya umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo MONUSCO imetoa wito wa kutendwa haki katika kesi dhidi ya afisa mmoja wa jeshi la Serikali aliyeasi na kutuhumiwa kwa uhaini.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa MONUSCO Florence Marchal amewaambia wanahabari jijini Kinshasa kuwa, tume yao inataka kuona haki inatendeka dhidi ya Kanali John Tshibangu ambaye majuma kadhaa yaliyopita alitishia kuipindua Serikali ya rais Joseph Kabila.

Umoja wa Mataifa unasema unafuatilia kesi yake kwa karibu huku ukisisitiza kuwa taratibu za namna Tshibangu alivyosafirishwa kutoka nchini Tanzania jumatatu ya wiki hii kutatoa picha ya namna haki itatendeka.

Kanali John Tshibangu alikamatwa kwenye uwanja wa ndege wa Dar es Salaam, nchini Tanzania na maafisa wa usalama wa nchi hiyo na kusafirishwa nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Mapem awiki hii Waziri wa Sheria nchini DRC Alexis Tambwe Mwamba alisema kuwa kuwa kesi Tshimbangu itasikilizwa kwa uwazi kama zilivyo kesi nyingine akithibitisha kuwa atashtakiwa kwa makosa ya uhaini.

Mke wa kanali Tshibangu, Mokee Tshibangu akiongea na idhaa ya Kiswahili ya RFI, alisema anahofia maisha ya mume wake na kuiomba Serikali isimchukulie mume wake kama muasi bali kama kamanda aliyeasi jeshi.