DRC-SIASA-MAANDAMANO

DRC: Kanisa Katoliki kuendelea kushinikiza kujiuzulu kwa rais Kabila

Polisi akirusha mabomu ya kutoa machozi kuwasambaratisha waandamanaji
Polisi akirusha mabomu ya kutoa machozi kuwasambaratisha waandamanaji SundiataPost

Viongozi wa Kanisa Katoliki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanasema, hawatachoka kuendelea kushinikiza kujiuzulu kwa rais Joseph Kabila.

Matangazo ya kibiashara

Mmoja wa viongozi wa Kanisa hilo Abbot Francois Luyeye amesema maandamano yataendelea kufanyika nchini humo katika siku zijazo.

Aidha, amesena kuwa Kanisa Katoliki linataka kuona DRC mpya na mabadiliko ya kisiasa nchini humo.

Kanisa hilo lemye nguvu nchini DRC, linamtaka rais Kabila ajiuzulu na kutangaza kuwa hatawania urais mwezi Desemba mwaka huu.

Rais Kabila ambaye muda wake wa kuendelea kuongoza kwa mujibu wa katiba umefika mwisho, hajasema iwapo atawania tena.

Kabila aliingia madarakani mwaka 2001. Amelishtumu Kanisa Katoliki kwa uchochezi wa kisiasa kwa lengo la kuwasaidia wanasiasa wa upinzani.