AFRIKA KUSINI-JACOB ZUMA

Hatima ya rais Zuma kufahamika siku ya Jumatatu

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma REUTERS/Sumaya Hisham

Kamati kuu chama tawala nchini Afrika Kusini, itakuna siku ya Jumatatu kujadili hatima ya rais Jacob Zuma ambaye anashinikizwa kujizulu kwa madai ya ufisadi, madai ambayo ameyakanusha.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa chama tawala cha ANC ambaye pia ni Naibu rais Cyril Ramaphosa amesema, raia wa Afrika Kusini wanataka suala hili kumalizika.

“Kamati kuu ya chama cha ANC itakutana kesho kujadili suala hili, kwa sababu watu wetu wanataka suala hili limalizike, kamati ya chama chetu itafanya hivyo,” alisema Jumapili.

Mkutano huo uliahirishwa wiki hii, baada ya kuwepo kwa ripoti kuwa kulikuwa na mazungumzo kati ya viongozi wa chama cha ANC n rais Zuma kuhusu uwezekano wa kuondoka kwake.

Ramaphosa alinukuliwa alikisema mazungumzo yalikuwa yanakwenda vizuri na mwafaka huenda ukafikiwa hivi karibuni.

Hata hivyo, rais Zuma ameendelea kukataa madai dhidi yake na kusema hakufanya kosa lolote na chama kinaweza kufanya lolote linalotaka ikiwa ni pamoja na kumwagiza aachane na urais.

Kumekua na maandamano kwa miezi kadhaa kumshinikiza Zuma ambaye amekuwa rais tangu mwaka 2009, kujiuzulu.