ETHIOPIA-MAANDAMANO-SIASA

Upinzani waendelea na mgomo Ethiopia

Maandamano ya upinzani katika mkoa wa Oromo, Ethiopia, Oktoba 2, 2016.
Maandamano ya upinzani katika mkoa wa Oromo, Ethiopia, Oktoba 2, 2016. REUTERS/Tiksa Negeri

Upinzani nchini Ethiopia unaendelea na mgomo wa siku tatu ulioanza tangu jana Jumatatu kushinikiza madai yao ya kuachiwa kwa wanasiasa wote na waandishi wanaoshikiliwa katika kipindi cha zaidi ya miaka miwili.

Matangazo ya kibiashara

Maandamano hayo yanafanyika katika mkoa ulio mkubwa nchini Ethiopia wa Oromia.

Mkoa wa Oromo ulikumbwa na machafuko katika kipindi cha miaka miwili.

Wakati huo huo serikali ya Ethiopia imesema itamwachilia huru kiongozi wa upinzani, Katibu Mkuu wa chama cha Oromo Federalist Congress, anayekabiliwa na ugonjwa, licha ya maandamano kuendelea katika baadhi ya maeneo ya nchi.

Mwendesha mashtaka mkuu nchini Ethiopia ametangaza kuwa serikali itamuondolea mashtaka ya kuchochea ghasia mwanasiasa huyo.

Alikamatwa Desemba, 2015 kwa mashtaka ya kuwa na mahusiano na makundi ya kigaidi. Lakini mashtaka hayo baadaye yalisbadilishwa na kushtumiwa uchochezi wa ghasia.

Hayo yanajiri wakati ambapo Serikali tayari imewaachia huru na kuwaondolea mashtaka maelfu ya watu, ikiwa sni ehemu ya mageuzi iliyoahidi kumaliza maandamano ya upinzani yaliyodumu kwa zaidi ya miaka mitatu nchini humo.

Jana Jumatatu, barabara nyingi ziliwekewa vizuizi na biashara kufungwa, huku shughuli nyingi zikizorota.