SUDANI KUSINI-OXFAM-HAKI

Oxfam yakabiliwa na mashitaka mapya ya ubakaji nchini Sudan Kusini

Wakimbizi hawa wa ndani wakipewa msaada wa chakula na shirika lisilo la kiserikali la Oxfam, Padding, Sudan Kusini, mnamo mwezi Julai 2017.
Wakimbizi hawa wa ndani wakipewa msaada wa chakula na shirika lisilo la kiserikali la Oxfam, Padding, Sudan Kusini, mnamo mwezi Julai 2017. AFP

Baada ya Haiti na Tchad, shirika la kihisani lisilo la kiserikali la Oxfam linaendelea kukumbwa na zimwi la ubakaji kwa wafanyakazi wake nchini Sudan Kusini na unyanyasaji wa kijsindia nchini Liberia. Hizi ni shutma mpya kwa shirika hili la misaada.

Matangazo ya kibiashara

Shutma hizi mpya zimeliweka mashakani shirika hili la Oxfam kwa shughuli zake duniani.

Helen Evans, Mkurugenzi wa masuala ya ndani ya Oxfam kati ya mwaka 2012 na 2015, ameshtumu kwenye kituo cha habari cha Channel 4 kuwepo kwa "tabia yaunyanyasaji wa kijinsia katika baadhi ya ofisi za Oxfam", huku akibaini kuepo kwa visa vya ubakaji au unyanyasaji wa kijinsia nchini Sudan Kusini au unyanyasaji kwa watoto wanafanya kazi kwa kujitolea katika ghala za shirika hilo nchini Uingereza.

Tuhuma hizi mpya zinakuja baada ya kufichuliwa kwa mvisa vya ukahaba na unyanyasaji wa kijinsia kwa wafanyakazi wa Oxfam nchini Chad na Haiti, ambapo Rais Jovenel Moise siku ya Jumanne, alishtumu "ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu". Wawakilishi wa Oxfam wameitishwa siku ya Alhamisi na wizara ya mipango na ushirikiano ya Haiti ili kutoa maelezo zaidi.

Pigo jingine kubwa kwa shirika hili ni kukamatwa kwa Mkuu wa Oxfam International nchini Guatemala. Waziri wa zamani wa fedha Juan Alberto Knight, alikamatwa siku ya Jumanne akishtumiwa kashfa ya rushwa isiyohusiana na kesi inayoendelea sasa.