Polisi yafanya msako nyumbani kwa marafiki wa Jacob Zuma

Ndugu kutoka familia ya Gupta, wenye asili ya India, wanashutumiwa na mamlaka ya kupambana na rushwa kutumia urafiki wao na Jacob Zuma ili kujijitajirisha.
Ndugu kutoka familia ya Gupta, wenye asili ya India, wanashutumiwa na mamlaka ya kupambana na rushwa kutumia urafiki wao na Jacob Zuma ili kujijitajirisha. REUTERS/Mike Hutchings

Polisi ya Afrika Kusini wamefanya msako leo Jumatatu nyumbani kwa ndugu kutoka familia tajiri ya Gupta, marafiki wa Rais Jacob Zuma, kama sehemu ya uchunguzi wa biashara kwa ushirikiano na Rais Zuma.

Matangazo ya kibiashara

Watu wawili wamekamatwa wakati wa msako huo mjini Johannesburg, kituo cha cha televisheni ya taifa SABC, kimeripoti.

Ndugu kutoka familia ya Gupta, wenye asili ya India, wanashutumiwa na mamlaka ya kupambana na rushwa kutumia urafiki wao na Jacob Zuma ili kujijitajirisha.

Hata hivyo familia hiyo imefutilia mbali shtma hizo, ikibaini kwamba hazina msingi.

Jana Jumanne chama tawala nchini Afrika Kusini, African National Congress (ANC), kilimtakaRais Jacob zuma atangaze mwenyewe jiuzulu la sivyo atang'olewa madarakani.

Jacob Zuma anatarajia kutoka jibu lake kuhusu kujiuzulu au la leo Jumatano.