DRC-BENI-USALAMA

Watu sita wauawa wilayani Beni baada ya kushambuliwa na waasi

Wanajeshi wa DRC wakiwa katika Operesheni dhidi ya waasi wa ADF NALU
Wanajeshi wa DRC wakiwa katika Operesheni dhidi ya waasi wa ADF NALU AFP PHOTO / ALAIN WANDIMOYI

Rais sita wa DRC wameuawa baada ya kushambuliwa na waasi katika eneo la Eringeti, Wilayani Beni Mashariki mwa nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa Mashirika ya kiraia wanasema watu hao walishambuliwa kwa kushtukizwa wakati walipokuwa wanatokea msibani.

Wanaharakati na maafisa wa Usalama wanasema, waasi wa ADF ndio waliohusika katika shambulizi hilo.

Katika hatua nyingine, Serikali nchini humo, imetangaza tahadhari ya mlipuko wa kipindupindu katika mkoa wa Mongala.

Serikali jijini Kinshasa inasema, ikishirikiana na Shirika la Afya duniani WHO, imetuma watalaam wa afya kwenda kuthathmini hali ilivyo.

Ripoti zinasema, maafisa waliwagunua watu waliokuwa na dalili za kipindupindu waliokuwa wanasafiria boti kutoka jijini Kinshasa kwenda mjini Kinsangati.