GAMBIA-HAKI

Adhabu ya kifo kufutwa Gambia

Rais wa Gambia Adama Barrow.
Rais wa Gambia Adama Barrow. REUTERS/Benoit Tessier

Rais wa Gambia ametangaza kwamba adhabu ya kifo haitorudi kutomika nchini humo. Tangazo hilo alilitoa jana Jumapili akibaini kwamba adhabu hiyo haiendani na wakati huu.

Matangazo ya kibiashara

Uamuzi wa kufuta adhabu ya kifo nchini Zambia unakuja mwaka mmoja baada ya rais dikteta wa zamani wa nchi hiyo Yhya Jammeh kutimuliwa madakani.

"Ninachukua nafasi hii kwa kutangaza hadharani kwamba adhabu ya kifo haitorudi kutumika nchini Gambia. Hii ni hatua ya kwanza kuelekea kufuutwa kwa adhabu hii, ", alitangaza adama Barrow wakati wa maadhimiso ya dmiaka 53 ya uhuru wa nchi hiyo.

Adhabu ya kifo imepungua katika nchi karibu zote za ukanda wa kusini mwa Sahara, ambapo watu 22 walinyongwa mnamo mwaka 2016 dhidi ya 43mwaka uliyotanguliwa (2015), kwa mujibu wa shirika la kimataifa la kutetea haki za binadam la Amnesty International.